Warsha ya roboti inawaangazia vijana wa Kenya kuhusu teknolojia za siku zijazo | Picha: Reuters

Vijana kutoka vitongoji duni vya Mathare, Nairobi, mji mkuu wa Kenya, walishiriki katika vikao vya mafunzo katika warsha ya Roboti iliyoandaliwa na shiriki lisio la kiserikali la Oasis Mathare Foundation mnamo Jumamosi (Mei 20).

Wakati wa warsha hio, vijana wengi ambao walihudhuria, walikuwa wakijishughulisha na kazi mbalimbali kuanzia mashine zinazotegemea vihisi pamoja na magari yanayoendeshwa na rimoti wakati wa mafunzo.

Sio vijana pekee bali hata wazazi pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli mbalimbali zilizotolewa wakati wa warsha.

Oasis Mathare ni shirika la kijamii linalowawezesha vijana na watoto waliotengwa kutoka katika vitongoji vya Mathare na huduma ya maktaba, ambapo watoto wanaweza kuja na kufanya masomo yao mbali na nyumbani ambapo wanakabiliwa na changamoto kama vile umeme kukatika na kutokuwa na nafasi ya kutosha ya kusoma.

Warsha hiyo ya roboti iliwapa wenyeji fursa ya kujihusisha na roboti -- fani ya uhandisi ambayo inahusisha kubuni, kuweka misimbo na kutengeneza roboti, kuwezesha uundaji wa mashine zinazosaidia watu kwa njia mbalimbali.

Reuters