Noti mpya ya 10000 BIF na ya zamani | Picha: TRT Afrika

Na Ferdinand Mbonihankuye

Walakini, watu, haswa wafanya biashara katika maeneo mbali mbali ya nchi ambapo benki na taasisi za kifedha ziko mbali wana wasiwasi kuwa kipindi hicho kitakuwa fupi mno.

Mpaka kufikia jana, tarehe 10 Juni, wale waliofika kuweka noti hizo walipokea noti za FBu 2,000 na FBu 1,000 tux.

Kuhusu hatua hii, baadhi ya watu katika maeneo ya mbali zaidi nchini Burundi ambapo benki na taasisi za mikopo hazipo karibu wana wasiwasi.

Wanalazimishwa kusafiri umbali mrefu kuweka noti hizo. Kwa benki fulani za mikopo kama Coopératives d'Epargne et de Crédit, COOPEC, na zingine, noti hazikuwa zinapatikana bado mpaka tarehe 8 Juni 2023.

"Ingawa hatua ya benki kuu ni nzuri, watu bado hawako tayari na muda ni mfupi sana." asema Alfred Igiraneza, mkazi wa wilaya ya Giharo, mkoa wa Rutana, kusini mashariki mwa Burundi, katika maongezi na TRT Afrika.

Iginareza asema uongezwe muda ili kuwezesha watu kuweka noti zao zote lasihivyo wataishia "kupoteza thamani ya hela yao".

Igiraneza anatuambia kuwa anasafiri takriban kilomita 128 kufika Sosumo ambapo kuna benki. Kuna watu ambao wanaweza kupoteza akiba zao aeleza.

Katika taarifa iliyotolewa tarehe 7 Juni 2023, Benki Kuu ya Jamhuri ya Burundi ilianzisha uondoaji katika mzunguko wa noti zote za FBu 10,000 na FBu 5,000.

Kwa sababu zilizotajwa na benki kuu, kuna ongezeko la usambazaji wa sarafu katika soko la kisiri, ambalo linaleta kutokuwa na utulivu katika shughuli za taasisi za kifedha ambazo hukusanya amana na kutoa mikopo.

Benki Kuu - Banque de la République du Burundi, BRB, pia inaelezea kuwa ukosefu wa noti za FBu 5,000 na FBu 10,000 katika hazina za benki na taasisi za fedha za mikopo unachangia kuzorota kwa shughuli za malipo na uhamishaji wa fedha. Gavana wa BRB alitangaza kuwa kuna uhaba nchini.

Ili kupata suluhisho, BRB imeamua kuziondoa katika mzunguko noti zilizotolewa tarehe 4 Julai 2018 na kuzibadilisha na noti mpya zilizotolewa tarehe 7 Novemba 2022. Noti hizo mpya zimeanza kutumika tarehe 7 Juni 2023.

Watu kutoka sehemu nyingine nchini pia wanapata shida kubadilisha noti hizo mpya. Katika ukurasa wao wa Twitter, Gazeti la Jimbere limeripoti leo kuwa noti mpya za Fbu 5,000 na 10,000 bado hazipatikani katika benki na taasisi ndogo za fedha zinazofanya kazi Bubanza, wateja wameeleza.

Wakati kipindi cha neema kilichotolewa na benki kuondoa kutoka kwa mzunguko noti za zamani za 5,000 Fbu na 10,000 Fbu inaisha baada ya siku 6 peke yake.

Ishara za kutambulisha noti hizo

Kulingana na benki kuu, noti mpya zitakuwa na ishara tano kuu. Noti za FBu 10,000 zitakuwa na rangi ya kijani na milia miwili ya kijani kwenye sehemu za chini na juu mbele na nyuma, nembo ya maji inayowakilisha picha ya Prince Louis Rwagasore ikiwa katika fremu ya mviringo inayoonekana, tarehe ya 7 Novemba 2022 na saini ya Gavana wa BRB na Naibu Gavana.

Kwa noti za FBu 5,000, rangi kuu ni kijivu na milia miwili ya rangi ya waridi kwenye sehemu za juu na chini, nembo ya maji inayowakilisha picha ya Rais Melchior Ndadaye iliyoko ndani ya fremu ya mviringo iliyofanywa kuwa wazi, nyuzi za usalama wa kijani na madirisha wazi zilizojumuishwa kwenye karatasi, tarehe ya noti ya 7 Novemba 2022 na saini ya gavana na naibu gavana wa BRB.

noti za zamani za 5000, 10000 BIF | Picha: Ferdinand Mbonihankuye

Watu ambao hawana akaunti wameombwa wafungue akaunti ili kuheshimu muda uliopewa. Kuanzia tarehe 18 Juni 2023, noti hizo hazitakuwa na thamani halali.

Benki kuu inakumbusha kuwa noti zilizotolewa tarehe 4 Julai 2018 zinaendelea kuwa na thamani halali hadi tarehe 17 Juni.

Maelekezo ya kuweka benki yameanzishwa

Benki Kuu ya Jamhuri ya Burundi inakumbusha kuwa noti zingine zilizotolewa kabla ya tarehe 4 Julai 2018 zitabadilishwa na noti mpya. Benki Kuu pia inasema kuwa amana zinadhibitiwa kama ifuatavyo.

Amana kwa mtu mmoja kwenye akaunti ya mtu binafsi ni FBu 10,000,000. Kwenye akaunti ya kisheria, jumla ya amana imezuiliwa hadi FBu 30,000,000 kwa siku na akaunti, na hatua hii haiwahusu Taasisi za Mikopo na Taasisi za Fedha za Mikopo zinazokusanya amana za umma na Wakala wa Posta wa Taifa.

Benki na Taasisi za Fedha za Mikopo zinaruhusiwa kubadilisha noti za FBu 5,000 na FBu 10,000 zilizotolewa katika mzunguko kwa kiwango kinachozidi FBu 100,000 kwa mtu. Kulingana na benki kuu, wale watakaopuuza hatua hii watashughulikiwa kulingana na kanuni na sheria zinazosimamia shughuli za benki.

Benki na taasisi za fedha za mikopo zimeombwa na benki kuu kuwezesha ubadilishaji wa noti za FBu 5,000 na FBu 10,000 zinazotolewa katika mzunguko kwa wateja wao ili kutekeleza hatua hii ya Benki Kuu ya Jamhuri ya Burundi.

Noti mpya ya 5000 BIF | Picha: Ferdinand Mbonihankuye

Kwa wakazi wa mkoa wa Kayanza, COOPEC na Wakala wa Posta wa Taifa, siku ya Ijumaa, walikuwa wakifanya tu malipo, na watu ambao walikuwa wamekuja kuweka noti zao za FBu 5,000 na FBu 10,000 hawakupokea noti mpya hizo.

Jibu la COOPEC na Wakala wa Posta wa Taifa lilikuwa kwamba watu hao warudi nyumbani na warejee COOPEC au posta wakati wanapopigiwa simu na kuarifiwa kuwa noti mpya za FBu 5,000 na FBu 10,000 zimepatikana.

TRT Afrika