SADC ilisema katika taarifa yake kwamba wanajeshi hao walipoteza maisha kufuatia shambulizi la kombora kwenye kambi yao./Picha: Getty      

Wanajeshi 4 wa Tanzania wameuwawa katika mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Askari hao ni sehemu ya majeshi la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yanayolinda amani nchini DRC.

Katika taarifa yake, SADC ilisema kuwa wanajeshi hao walipoteza maisha yao kufuatia shambulizi la kombora kwenye kambi yao.

"Tukio hili la kusikitisha limetokea baada ya kombora kurushwa kwenye kambi yao," SADC imesema.

Sehemu ya majeshi ya SADC yakiwa katika doria za kawaida nchini DRC./Picha: TRT Afrika.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya mataifa 10 ambayo yanashirikiana kurejesha amani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Vikosi vya SADC vinachukua nafasi ya majeshi ya kulinda amani kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) ambavyo vilimaliza muda wake mwaka jana.

TRT Afrika