Moïse Katumbi. nimiongoni mwa zaidi ya wagombea 20 wanaotafuta urais wa nchi hiyo yenye zaidi ya wapiga kura milioni 43 Picha : Reuters

Wagombea wawili wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi ujao walisema Jumatatu kwamba watajiondoa na kumuunga mkono mgombea mwingine wa upinzani, Moise Katumbi, kufuatia hatua iliyochukuliwa na mgombea mwingine wiki iliyopita.

Seth Kikuni na Franck Diongo ni wagombea wa hivi punde wa upinzani kutoa uungwaji mkono wao nyuma ya Katumbi mwenye umri wa miaka 58, mfanyabiashara milionea na gavana wa zamani wa eneo lenye utajiri wa shaba la Katanga.

Hii inafuatia mkutano wa waakilishi wa vyama vyao nchini Afrika Kusini wiki jana kujadili jinsi ya kulinda uchaguzi mkuu wa Desemba 20 dhidi ya udanganyifu na kuamua kuhusu mgombea mwenza anayetarajiwa kumpinga Rais Felix Tshisekedi, 60.

Punde baada ya kumalizika kikao hicho Jumapili Waziri mkuu wa zamani wa Congo Augustin Matata Ponyo alisema atamuunga mkono Katumbi kufuatia mapendekezo ya viongozi wa vyama vya upinzani.

Kampeni ya Katumbi ilianza rasmi Jumatatu katika mji wa Kaskazini wa Kisangani. Ameahidi kupambana na ufisadi, kuunda nafasi za kazi na mageuzi ya uchumi wa mzalishaji mkubwa zaidi wa vifaa vya betri duniani cobalt na mzalishaji mkuu wa shaba.

Uchaguzi huo wa Disemba 20 umewavutia wagombea zaidi ya 20 wanaotafuta kumpinga Rais aliye madarakani sasa hivi Felix Tshisekedi ambaye anawania muhula wake wa pili iwapo atafanikiwa.

Wapinzani wake wakuu ni pamoja na Katumbi, mpinzani wa zamani Martin Fayulu, mtendaji wa zamani wa Exxon Mobil mwenye umri wa miaka 66 ambaye aliibuka wa pili katika kinyang'anyiro cha urais kilichopita 2018, na mgombea wa mara ya kwanza Denis Mukwege, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel.

Kumekuwa na madai ya wasiwasi kuhusu haki ya kura, huku baadhi ya wagombea wa upinzani wakidai kuwa kuna kasoro ambazo zinaunga mkono muungano unaotawala wakati wa usajili wa wapigakura. Tume ya uchaguzi inakanusha hili.

TRT Afrika