| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Wagombea 11 wapewa tikiti kuwania urais nchini Zimbabwe
Tume ya uchaguzi iliwataka wagombea wote kulipa dola 20 000 ili kuruhusiwa kujumuishwa majina yao katika karatasi za kura ya urais
Wagombea 11 wapewa tikiti kuwania urais nchini Zimbabwe
Aliyekuwa mgombea wa pekee wa kike katika uchaguzio wa rais alikosa kulipa ada inayotakiwa / Picha: Reuters / Reuters
23 Juni 2023

Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe imewaidhinisha wagombea 11 kuwania urais katika uchaguzi wa Agosti.

Tume hiyo inasema kuwa watu 11 wengine walikosa tikiti katika uchaguzi huo akiwemo Linda Masarira, mgombea wa pekee wa kike, kwa kushindwa kutimiza mahitaji muhimu ikiwemo kukosa kulipa ada ya dola 20,000 inayotakiwa kulipwa kabla kuongezwa jina lako katika karatasi za kura.

“Nimeweka wazi kuwa hizo dola 20,000 ni kubwa mno, ni za kibaguzi na zinakiuka kifungu kinachozungumzia kutobagua mbele ya sheria,” Masarira aliambia shirika la Reuters.

Ushindani mkali unatarajiwa kati ya rais wa sasa Emmerson Mnangagwa wa chama cha ZANU-PF, na mchungaji na wakili Nelson Chamisa wa Chama cha Wananchi (CCC)

Mnangagwa, 80, anatafuta muhula mwingine huku kukiwa na kuzorota kwa uchumi, huku dola ya Zimbabwe ikiporomoka kwa zaidi ya 50% mwezi huu dhidi ya dola ya Marekani.

Akizungumzia wanahabari baada ya kupata cheti chake katika mahakama ya juu, Mnangagwa alisema utaratibu wote unaonesha kukomaa kwa demokrasia ya Zimbabwe.

Kwa upande wake Chamisa, amesema kuwa ana matumaini katika uchaguzi ujao baada ya kunusia kwa karibu zaidi katika uchagzui uliopita na kushindwa.

Zimbabwe inatarajiwa kupiga kura ya rais na wabunge Agosti 23.

CHANZO:TRT Afrika, Reuters