Wafuasi sita wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini, wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea siku ya Jumamosi, katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.
Katika taarifa yake, Chama hicho cha uMkhonto Wesizwe (MK) Party kimeoneshwa kusikitishwa na ajali hiyo.
Watu wengine kumi walijeruhiwa na kuwahishwa hospitalini, ilisema taarifa ya Chama hivho kilichoasisiwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Ajali imetokea wakati wafuasi wa Chama cha MK wakiwa safarini kuelekea Nkandla katika jimbo la Kwa-Zulu Natal.
Usalama barabarani
Licha ya kuwa na mtandao bora wa barabara katika bara la Afrika, Afrika Kusini inaongoza kwa ajali za barabarani, zinazosababishwa na uzembe wa madereva na ubovu wa magari.
Mapema wiki hii, basi lililokuwa linasafiri kati ya Zimbabwe na Afrika Kusini, lilipinduka na kuua watu 10 na kujeruhi wengine 35, katika jimbo la Limpopo, lililo kusini mwa nchi hiyo.