Msumbiji ilikumbwa na hali ya vurugu kufuatia uchaguzi wa Oktoba 9./Picha: AP

Wabunge 250 wamekula kiapo siku ya Jumatatu huku hali ya kawaida ikianza kurejea nchini humo.

Hata hivyo, vyama vikuu vya upinzani nchini Msumbiji Renamo na Democratic Movement vikisusia shughuli hiyo, vikipinga uchaguzi wa Oktoba 9.

Kulingana na Margarida Talapa, ambaye alichaguliwa spika wa bunge la nchi hiyo, wabunge wataendelea kufanya jitihada za kurejesha utulivu wa kisiasa nchini Msumbiji.

Talapa, ambaye ni mwanachama wa Frelimo alichaguliwa spika wa bunge la nchi hiyo baada ya kushinda kwa kura 160.

TRT Afrika