DRC imeshuhudia ukosefu wa usalama unaoendelea, haswa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. / Picha: AFP

Raia walikuwa wanakimbia Alhamisi wakati waasi wa M23 walipokuwa wakikaribia mji mwingine wa kimkakati katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vyanzo vya ndani vimesema.

Vuguvugu la Machi 23 lilianza tena vurugu mwishoni mwa mwaka 2021, likitwaa maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Jeshi la Kongo limejaribu kupambana na kundi la waasi, ambalo limeuzingira mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, ambako mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wamepata hifadhi.

Waasi walikuwa sasa wanakaribia mji wa Kanyabayonga, ambao uko kwenye barabara kuelekea Goma.

Hali 'mbaya sana'

"M23 iko kilomita tano kutoka katikati ya Kanyabayonga," afisa wa eneo hilo aliambia AFP kwa njia ya simu.

"Kanyabayonga iko kwenye mchakato wa kuachwa bila watu," chanzo kingine kilisema.

"Hali ni mbaya sana na watu wameanza kukimbia" kuelekea kaskazini, afisa asiyejulikana alisema.

Goma iko njia ya kuelekea miji muhimu ya Butembo na Beni na ina watu wapatao 60,000, mbali na makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao ambao wamepata hifadhi hapo.

Watu wanakimbia

Mapigano pia yaliripotiwa Alhamisi katika eneo la Masisi karibu na Sake, ambalo liko kilomita 20 tu magharibi mwa Goma.

FARDC, au majeshi ya silaha ya Kongo, yakisaidiwa na wanamgambo wenye silaha wanaojulikana kama Wazalendo – walizindua shambulio wiki moja iliyopita katika maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini kwa nia ya kurejesha maeneo yaliyochukuliwa na M23.

M23 ilitwaa mji wa Kyaghala Jumatatu, afisa wa jamii ya kiraia alisema, na kuongeza kuwa hili lilisababisha watu kukimbilia Kanyabayonga.

AFP