Viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria wamesitisha mgomo wao, japo kwa muda, ili kupisha mazungumzo ya kuongeza kima cha chini cha mshahara.
Usitishwaji huo uliratibiwa na NCL na TUC siku ya Jumanne, huku nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ikikabiliana na mfumuko wa bei na kutokuimarika kwa sarafu ya Naira.
Jumatatu jioni, serikali ya nchi ilisema kuwa vyama vya wafanyakazi vilikubali wiki nyingine ya mazungumzo kujaribu kufikia makubaliano juu ya mshahara.
Baada ya majadiliano na wanachama siku ya Jumanne, NLC na TUC wameamua kusitisha mgomo kwa siku saba.
"Tumelegeza kidogo maamuzi yetu kwa wiki moja ili kuruhusu kukamilika kwa majadiliano," ilisema NCL kupitia ukurasa wake wa X.
Sharti la kuongeza mshahara
Vyama vya ushirika nchini humo vinataka ongezeko la chini cha mshahara wa mwezi kutoka dola 20.17 hadi dola 330.
Jumatatu jioni, serikali ya Nigeria ilisema kuwa iko tayari kutoa naira 60,000 kama mshahara wa kima chini na kwamba pande hizo mbili zitakutana "kila siku kwa wiki ijayo" ili kufikia makubaliano.
Vyama hivyo vimepigia kelele ongezeko katika gharama za umeme, ambalo ni moja ya maboresho ya Rais Bola Ahmed Tinubu.
Tangu aingie ofisini mwaka mmoja uliopita, Tinubu amemaliza ruzuku ya mafuta na udhibiti wa sarafu, na kusababisha kupanda mara tatu kwa bei ya petroli na kupanda kwa gharama za maisha huku naira ikishuka dhidi ya dola.
Serikali imewataka Wanigeria kutoa muda kwa mageuzi hayo kufanya kazi, ikisema yatavutia uwekezaji zaidi kutoka nje, lakini hatua hizo zimeathiri matumizi makubwa ya nguvu.
Siku ya pili ya mgomo ilikuwa imechanganyika zaidi ya Jumatatu.
Huko Abuja, baadhi ya wafanyikazi wa wizara walirejea kazini ingawa ofisi nyingi na jengo la Bunge la Kitaifa bado lilikuwa limefungwa, kama ilivyoshuhudiwa na waandishi wa AFP.
Wafanyakazi kutoka sekta ya anga walikusanyika nje ya lango lililofungwa la uwanja wa ndege wa ndani wa Lagos, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo.
Hata hivyo, huduma za ndege za kimataifa bado zilikuwa zikiendelea siku ya Jumanne, msemaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Shirikisho la Nigeria alisema.
Wachezaji wanane wa timu ya taifa ya Nigeria ya Super Eagles, akiwemo winga Ademola Lookman, walikwama siku ya Jumatatu kutokana na hitilafu za ndege na hawakuweza kufanya mazoezi ya kufuzu Kombe la Dunia, msemaji wa timu alisema.