Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania imevitaka vyama ambavyo havijachaguza viongozi wake kufanya hivyo, kabla muda kuisha.
Hii ni kufuatia ofisi hiyo kubaini uwepo wa idadi kubwa wa vyama vya siasa ambavyo muda wa viongozi wake kukaa madarakani umefikia kikomo, kufikia mwaka huu.
"Kwa mujibu wa sheria, kila chama cha siasa kinapaswa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia wa viongozi wake kwa vipindi ambavyo vimewekwa katika Katiba yake...vilevile uchaguzi wa viongozi wa chama cha siasa unapaswa kufanyika sio zaidi ya miaka mitano tangu uchaguzi uliopita kufanyika," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Tanzania ina jumla ya vyama vya siasa 19, vyenye usajili kamili kutoka ofisi hiyo.
TRT Afrika