Visa vya kipindupindu nchini Msumbiji vilizidi 10,000 siku ya Jumapili katika wimbi ambalo limekumba taifa hilo la kusini mwa Afrika tangu kuanza kwa mlipuko huo mwezi Oktoba, kulingana na Kurugenzi ya Kitaifa ya Afya ya Umma.
Shirika hilo, ambalo linatathmini habari za afya ya umma hadi Januari 21, lilibaini kuwa kumekuwa na kesi 10,061 tangu mwanzo wa Oktoba.
Kati ya kesi zilizorekodiwa, wahasiriwa 25 wamekufa na 7,321 wamelazwa hospitalini, ilisema.
Nchi jirani ya Zimbabwe haikurekodi vifo vyovyote vya kipindupindu katika wiki mbili zilizopita, kulingana na takwimu rasmi.
Kampeni ya kutoa chanjo
Mamlaka ya Msumbiji imetambua karibu wilaya 30 ambazo zinakabiliana na visa vya ugonjwa wa kipindupindu na Mkoa wa Nampula kaskazini unashika nafasi ya juu zaidi, na visa 3,246 na vifo 12.
Ndani ya siku tano baada ya mlipuko wa ugonjwa huo, mamlaka nchini Msumbiji imetoa chanjo kwa watu milioni 2.2 katika wilaya zilizoathirika zaidi dhidi ya janga ambalo linaendelea kusababisha maafa.
Kampeni ya chanjo ya Msumbiji ililenga watoto wenye umri wa miaka 1 na zaidi. Ilifanyika katika wilaya za Chiure na Montepuez (mkoa wa Cabo Delgado), Gile, Gurue na Mocuba (Zambezia), Magoe, Moatize na Zumbo (Tete) na Meringue (Sofala).
Kampeni ya chanjo ya taifa la Afrika ilikusanya timu 1,136 zenye wafanyakazi 7,337, wakiwemo watoa chanjo, wahamasishaji, wasajili, wasimamizi, waratibu, wafanyakazi wa kuingiza data, wataalamu wa vifaa na madereva, ambao gharama yao ilikuwa karibu dola milioni 1.3.