Tangu kuanza kwa mwaka huu, Afrika Kusini imerekodi ongezeko la visa vya homa hiyo huku nchi hiyo ikiingia msimu wa baridi. / Picha: Reuters

Idadi ya maambukizi ya homa ya mafua Afrika Kusini imeongezeka sana katika siku chache zilizopita, idara ya afya ya nchi hiyo inasema.

Idara hiyo ilisema katika taarifa ya hivi majuzi kwamba visa vya homa ya mafua, inayojulikana kama flu imeripotiwa zaidi mashuleni na sehemu za kazi.

Mafua ni ugonjwa wa kupumua unaoambukiza unaosababishwa na virusi vya mafua ambayo huambukiza pua, koo, na wakati mwingine mapafu.

KwaZulu-Natal, Mpumalanga, Gauteng, Western Cape, Eastern Cape na North West ni majimbo ambayo yamethibitisha kuzuka kwa ugonjwa huo.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, Afrika Kusini imerekodi ongezeko la visa vya homa hiyo huku nchi hiyo ikiingia msimu wa baridi.

Wakati huo huo, Idara ya Afya ilithibitisha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa malaria, na uchunguzi mwingi ulifanywa katika hatua za baadaye. Kwa wastani, Afrika Kusini inarekodi kati ya visa 10,000 na 30,000 vipya vya malaria kila mwaka.

Kipindupindu, ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kawaida huenezwa kupitia maji au chakula kilichochafuliwa, pia umethibitishwa nchini humo, huku takriban watu 26 wakiugua ugonjwa huo, kulingana na rekodi rasmi.

TRT Afrika