Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso akiwasili kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara, Uturuki mnamo Juni 03, 2023 / Picha: AA

Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Shirika la Nchi za Kituruki (OTS), NATO, na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watakuepo pia.

Marais wa Kongo Brazzaville, Gabon, Somalia na Guinea walifika Ankara siku ya Ijumaa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa.

Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba Picha AA

Erdogan atachukua kiapo katika Bunge la Kitaifa la Uturuki saa 8:00 mchana saa za Uturuki na ataanza muhula wake mpya. Atapokea mamlaka yake kutoka kwa Spika Muda wa Bunge la Kitaifa la Uturuki, Devlet Bahceli.

Erdogan alishinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 28 Mei baada ya kupata asilimia 52.18 ya kura dhidi ya mgombea wa upinzani Kemal Kilicdaroglu aliyepata asilimia 47.82.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliwasili mjini Ankara kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais Recep Tayyip Erdoğan.

Uchaguzi ulipelekwa katika duru ya pili baada ya wagombea wa urais kutoshinda asilimia 50 plus moja ya kura katika uchaguzi wa Mei 14, ingawa Erdogan alikuwa anaongoza vizuri katika duru ya kwanza.

TRT Afrika