Takriban watu 21 wamepoteza maisha katika vurugu zilizotolea baada ya mahakama ya juu nchini Msumbiji kuthibitisha ushindi wa mgombea wa chama tawala cha Frelimo Daniel Chapo katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 9 unaopingwa na wengi, imesema Wizara ya Mambo ya ndani Jumanne.
“Jumla ya vitendo vya vurugu 236 vimeripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ambapo watu 25 wamejeruhiwa na wengine 21 kupoteza maisha,” Pascoal Ronda amewaambia waandishi wa habari.
Vifo vya hivi karibuni vimeongeza idadi hiyo na kufikia watu 151 tangu Oktoba 21, baada ya maandamano mabaya kutokea baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza Chapo mshindi wa uchaguzi, kwa mujibu wa Plataforma Decide, kundi linalofuatilia uchaguzi.
Punde tu baada ya Tume ya Katiba ambayo ina mamlaka ya juu ya mambo yote yanayohusiana na uchaguzi katika taifa hilo la lililopo kusini mwa Afrika, kuthibitisha ushindi wa Chapo, maelfu ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani anayeishi uhamishoni Venancio Miondlane waliingia barabarani kupinga matokeo.
Waandamanaji wanatuhumiwa kuharibu vituo vya polisi na taasisi nyengine za umma.
Jumatatu, benchi ya mahakimu saba wa Tume ya Katiba walithibitisha tangazo la awali lililotolewa na tume ya uchaguzi na kumtangaza Chapo kuwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 9, lakini kupunguza asilimia ya ushindi wake kutoka 71 hadi 65.
Siku chache kabla ya mahakama kutoa uamuzi, Mondlane ambae ambae amejipeleka uhamishoni mwenyewe, aliwaonya raia kwa “siku ngumu mbeleni.”