| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Vifo baada ya mapigano ya jeshi la Sudan, na RSF Darfur kaskazini
Takriban watu watatu wamethibitishwa kufariki na wengine 12 kujeruhiwa katika eneo la Darfur Kaskazini mwa Sudan katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.
Vifo baada ya mapigano ya jeshi la Sudan, na RSF Darfur kaskazini
Mwanajeshi wa Sudan akitazama huku akiwa ameshikilia silaha yake barabarani huko Omdurman, Sudan, Machi 9, 2024. REUTERS / Others
1 Aprili 2024

Takribani watu watatu waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika mapigano kati ya vikosi vya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko Al-Fasher katika jimbo la Darfur Kaskazini, kulingana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.

Katika taarifa, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema majeruhi walitokea wakati ndege za kivita zilishambulia maeneo yaliyo na wanamgambo wa RSF katika mji huo magharibi mwa Sudan.

Hakukuwa na maoni kutoka kwa jeshi la Sudan kuhusu ripoti hiyo.

Sudan imekumbwa na mapigano kati ya jeshi, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza Tawala la Ufalme, na RSF.

Maelfu Wauawa

Takribani watu 13,900 wameuawa na zaidi ya milioni nane kukamishwa kutoka makwao katika mgogoro ulioanza Aprili 2023, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Saudi Arabia na wapatanishi wa Marekani yameshindwa kumaliza vurugu.

Pata Habari Zaidi kupitia WhatsApp channels

CHANZO:TRT Afrika na mashirika ya habari