Sekunde chache tu kabla ya roketi ya Falcon 9 ambayo imebeba Setilaiti ya Kenya ‘Taifa 1’ kuzinduliwa shughuli hiyo ilisitishwa.
"Usitishaji huo umelazimika kwa sababu ya mwenendo wa hali ya hewa… gari na mzigo wa malipo ya kwenda angani unaendelea kuwa katika afya njema na fursa yetu inayofuata ya uzinduzi ni kesho wakati huo huo (9.48am Afrika Mashariki)" Kampuni ya SPACE X iliyosimamia uzinduzi huo ilisema.
‘Taifa 1’ ni setilaiti ya kwanza ya uchunguzi wa dunia nchini Kenya. Shirika la Anga za Juu la Kenya linasema kuwa setilaiti hiyo itachukua picha zitakazotumika kufuatilia hali ya hewa, mafuriko, hali ya mazao na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na maliasili.
Satelaiti hiyo iliundwa na kutengenezwa na wahandisi 9 wa Kenya na imegharimu nchi takriban $370,000.
Uzindizi wa ‘Taifa 1’umeahirishwa mara mbili hapo awali kwasababu ya hali mbovu ya hewa.
Ucheleweshaji huo pia unaathiri kuzinduliwa kwa setilaiti ya kwanza ya uchunguzi wa ardhi ya Uturuki iliyojengwa nchini humo,IMECE. Setilaiti hiyo yenye ubora wa juu pia itarushwa ndani ya roketi ya Falcon 9.