Uturuki yalenga kuongeza uhusiano wa kibiashara na nchi za Asia-Pasifiki

Uturuki yalenga kuongeza uhusiano wa kibiashara na nchi za Asia-Pasifiki

Ziara ya Erdogan nchini Malaysia, Indonesia na Pakistan inalenga kukuza ushirikiano na miradi mingine.
Rais huyo wa Uturuki atakuwa pia mwenyekiti mwenza wa Baraza la Ushirikiano la Ngazi ya Juu nchini na viongozi wenzake wa Indonesia na Pakistan./Picha: AA

Uturuki inalenga kukuza uhusiano wa kibiashara na Asia-Pasifiki wakati Rais Recep Tayyip Erdogan akijiandaa na ziara yake ya bara la Asia.

Kulingana na Nail Olpak, ambaye ni rais wa bodi ya uhusiano wa biashara ya nje ya Uturuki (DEIK), ujazo wa kibiashara kati ya Uturuki na nchi za Malyasia, Indonesia na Pakistan umevuka dola bilioni 8, huku Erdogan akianza na ziara yake ya siku tatu katika bara la Asia siku ya Jumatatu.

Rais huyo wa Uturuki atakuwa pia mwenyekiti mwenza wa Baraza la Ushirikiano la Ngazi ya Juu nchini na viongozi wenzake wa Indonesia na Pakistan.

Wakati wa ziara hiyo, Erdogan anatarajiwa kutia saini makubaliano mbalimbali katika masuala kadhaa pamoja na kukutana na jumuiya ya wafanyabiashara katika nchi hizo tatu, mkazo ukiwa masuala ya kikanda, kiulimwengu, hususani suala la Gaza.

DIEK imelenga kuwaalika wawakilishi wa kibiashara kutoka Uturuki, wakati wa ziara hiyo.

Kulingana na Olpak, bodi hiyo itakuwa na vikao maalumu na kila nchi pamoja na baraza la biashara siku ya Jumanne jijini Kuala Lumpur, ukifuatiwa na mwingine jijini Jakarta siku ya Jumatano, kabla ya kuhitimisha na wa Islamabad siku ya Alhamisi."

Ulimwengu wa diplomasia ya uchumi

DEIK inaendeleza diplomasia yake ya kiuchumi, ikishirikiana na taasisi mbalimbali ulimwenguni. Kulingana na Olpak, ushirikiano huo "utawaleta pamoja wafanyabiashara wetu kufanya tathmini ya fursa za kibiashara na uwekezaji."

Bodi hiyo inalenga kuongeza miradi ya Uturuki na uhusiano wa kibiashara na Malaysia, Indonesia na Pakistan. Kwa sasa, ujazo wa kibiashara unafikia dola bilioni 5, zaidi ya dola bilioni 2 na dola bilioni 1, mtawalia.

"Maeneo ambayo tunalenga kukuza ushirikiano ni pamoja na sekta ya ulinzi, anga, nishati, miundombinu, ujenzi, elimu, afya, kilimo, utalii, uchumi wa kidijiti, na mengineyo," aliongeza Olpak.

"Pia tunalenga kuongeza uhusiano wetu wa kitamaduni na kiuchumi."

TRT Afrika