Uturuki imelaani 'vitendo vya kusudi vya vurugu' na mauaji yampiga picha alikuwa akilifanyia kazi kutoka Gaza Shirika la Kimataifa la Uturuki Anadolu kama mwandishi wa kujitegemea.
"Maelfu ya watu wasio na hatia wamepoteza maisha yao katika mauaji ya halaiki ya miezi miwili yaliyofanywa na Israeli. Ikizingatiwa kwamba, waandishi 72 waliokuwa wakitekeleza majukumu yao miongoni mwa watu wasio na hatia ambao wamepoteza maisha yao ni dhahiri kwamba Israeli inashambulia uhuru wa watu wa kupata taarifa," Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun amesema kupitia mtandao wa X siku ya Ijumaa.
Kauli yake, imekuja punde tu baada ya mpiga picha wa kujitegemea wa Anadolu Montaser Al-Sawaf aliuawa kutokana na shambulizi la anga la Israel.
"Jumuia ya kimataifa na jumuia ya wanaandishi wa habari lazima ichukue hatua madhubuti bila kuchelewa kusitisha mauaji haya ya halaiki haraka iwezekanavyo.
"Kwa mara nyengine tunalaani mauaji ya halaiki ya Israeli na vitendo vya makusudi vya vurugu dhidi ya waandishi wa habari ambayo zinasababisha vifo," amesema Altun.
Pia ametoa salamu zake za rambirambi kwa familia ya Al-Sawaf, wenzake, na Anadolu.