Erdogan amezungumza katika mpango wa  'Mabadiliko ya Karne Istanbul' uliofanyika katika Kituo cha Maonyesho cha Ukumbi wa Kimataifa wa Lutfi Kirdar jijini Istanbul. / Picha: AA  

Uturuki imejipanga kuzuia "muundo wa kigaidi" kuchipua pembezoni mwa mipaka yake ya kusini, rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan amethibitisha.

"Kwa gharama yoyote, Uturuki haitaruhusu kuwepo kwa taasisi ya kigaidi kaskazini mwa Iraq au kaskazini mwa Syria," Erdogan amesema, akihutubia katika shughuli iliyofanyika jijini Istanbul Jumamosi.

Kauli yake inakuja baada ya wanajeshi sita wa Uturuki kuuawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi la PKK/YPG karibu na mpaka wa kaskazini na Iraq Ijumaa.

Magaidi wa PKK mara nyingi wanajificha katika mpaka kaskazini ya Iraq ili kupanga mashambulizi ya kigaidi nchini Uturuki.

Akitoa salamu zake za rambirambi ya vifo vya wanajeshi hao, Erdogan ametangaza kwamba, tangu ya shambulio, magaidi12 "wamekatwa makali" katika oparesheni ya kaskazini mwa Iraq, na kaskazini mwa Syria.

"Ndani ya Oparesheni hiyo kaskazini ya Syria, jumla ya magaidi 12 wamekatwa makali mpaka sasa," Erdogan amesema.

Mamlaka ya Uturuki inatumia neno "kukata makali" ikimaanisha kwamba magaidi wanaohusika aidha wamejisalimisha, wameuawa au kushikwa.

Katika kampeni yake ya kigaidi ya zaidi ya miaka 35 dhidi ya Uturuki, PKK — ambayo imeorodheshwa kama taasisi ya kigaidi na Uturuki, Marekani, na Umoja wa Ulaya— imehusika na mauaji ya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake, watoto na watoto wachanga.

TRT World