Putin ametaka usitishwaji wa mapigano na Moscow kwa mara kadhaa imekosoa mwenendo wa Isaeli Gaza baada ya shambulizi ya Oktoba 7.  / Picha: Reuters  

Urusi imeialika Hamas na makundi mengine ya Palestina ikiwemo Fatah kwa ajili ya mazungumzo dhidi ya mashambulizi ya Israeli Gaza na mambo mengine yanayohusu Mashariki ya Kati, taarifa rasmi imesema.

Urusi imeyaalika makundi kadhaa ya Palestina katika kila inachokiita, mazungumzo ya "Palestina" kuanzia Februari 29, Shirika la Habari la Taifa la TASS limeripoti Ijumaa, likimnukuu Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mikhail Bogdanov.

"Tumewaalika wawakilisha wote wa Palestina- wawakilishi wote wa kisiasa wenye nafasi mbalimbali nchini, ikiwemo Syria, Lebanon na nchi nyengine katika kanda," amesema Bogdanov, ambae ni mjumbe maalumu wa Rais Vladimir Putin katika Mashariki ya Kati.

Mwaliko huo umejumuisha Hamas, na kikundi cha Palestina cha Islamic Jihad, pamoja na wawakilishi wa Fatah pamoja na PLO.

Tangu Oktoba 7, Israeli imeua takriban Wapalestina 28,775 waliopo Gaza, wengi wao, wakiwa ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina katika eneo lililozingirwa.

Putin ameitisha kusitishwa kwa mapigano huku Moscow mara kadhaa ikikosoa mwenendo wa Israeli ndani ya Gaza baada ya shambulizi ya Oktoba 7.

Taarifa hiyo ya umma, iliyounganisha washiriki wa Urusi pamoja na Iran na Hamas, imetibua uhusiano kati ya Urusi na Israeli tangu mgogoro huo kuibuka.

TRT World