Takriban watoto 100,000 wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Morocco Ijumaa iliyopita, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilisema.
''Wakati UNICEF bado haijafahamu idadi kamili ya watoto waliouawa na kujeruhiwa, makadirio ya hivi punde kutoka 2022 yanaonyesha kuwa watoto wanawakilisha karibu theluthi moja ya watu nchini Morocco,'' shirika hilo lilisema katika taarifa yake Jumatatu.
Zaidi ya watu 300,000 wameathiriwa huko Marrakech na katika Milima ya Juu ya Atlas kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8, kulingana na makadirio ya UN.
Zaidi ya watu 2,800 wameuawa, wakiwemo watoto, huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa, ilisema Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.
Uharibifu mkubwa
Mamlaka zinahofia kuwa huenda idadi hii ikaongezeka.
Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS) limesema kitovu cha tetemeko hilo lililotokea baada ya saa tano usiku, saa za ndani (2200GMT), ilikuwa kilomita 75 (maili 46.6) kusini magharibi mwa Marrakech kwa kina cha kilomita 18.5 (maili 11.5).
Uharibifu mkubwa uliripotiwa huko Marrakech, eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, kutokana na tetemeko hilo kuu.
Takriban watoto 100,000 wameathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Morocco Ijumaa iliyopita, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) lilisema.
Vikosi vya uokoaji siku ya Jumatatu viliendelea kuwatafuta watu waliopotea waliokwama chini ya vifusi kwa siku ya tatu kufuatia tetemeko hilo baya.
Timu kadhaa za uokoaji za kigeni tayari zimewasili nchini ili kuungana na juhudi za kuwaokoa manusura.
Morocco hadi sasa imekubali matoleo ya usaidizi kutoka Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Siku ya Jumapili, serikali ya Morocco ilizindua akaunti maalum na hazina na Benki Kuu ya Morocco ili kupokea michango kwa ajili ya waathirika wa tetemeko hilo.
Tetemeko hilo lilikuwa kubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ya Afrika Kaskazini katika karne iliyopita, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Jiofizikia ya Morocco.