Ugandan tourists killed by unknown assailants

Uganda imesema siku ya Alhamisi kuwa imemkamata mkuu wa kikosi cha wanamgambo kilicholaumiwa kwa mauaji ya watalii wawili wa kigeni waliokuwa katika fungate pamoja muongoza wageni katika mbuga ya kitaifa mwezi uliopita.

Kiongozi huyo pekee ndie aliyesalimika katika operesheni ya kijeshi ya usiku wa Jumanne dhidi ya wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) iliyowaua wapiganaji wengine sita, jeshi lilisema.

Raia hao wawili wa kigeni waliuawa pamoja na msaidizi wao katika shambulio la Oktoba 17 wakiwa safarini katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth.

Uganda ilililaumu kundi la wanamgambo wenye silaha ADF, lililoko Katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaloshirikiana na kundi Daesh.

Baadaye kundi la hilo lilitangaza kuhusika kwenye shambulio hilo, likisema kuwa liliua "watalii watatu wakristo."

Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Deo Akiiki aliliambia Shirika la Habari la AFP kuwa kamanda wa kitengo hicho, aliyejulikana tu kama Njovu, alijeruhiwa mgongoni wakati wa mapigano ya bunduki siku ya Jumanne.

"Hii ilikuwa operesheni iliyofanikiwa ya pamoja ikiongozwa na ujasusi wa kijeshi na kikosi chote kilichotumwa na ADF kusababisha ghasia, kuua watalii, kuchoma shule, hospitali, kiliondolewa," Akiiki alisema.

"Aliyenusurika pekee ni kamanda tuliyemkamata," alisema, akiongeza kuwa alikuwa akitibiwa katika eneo la siri na atakabiliwa na mashtaka.

Akiiki alisema Njovu alipatikana na baadhi ya mali za watalii waliouawa na kitambulisho cha muongoza watalii wao wa Uganda.

Waathirika wa shambulio la Oktoba wametajwa kuwa raia wa Uingereza David Barlow, mkewe wa Afrika Kusini Celia na mwelekezi, Eric Ayai.

Meja Jenerali Dick Olum, anayesimamia operesheni za kijeshi za Uganda dhidi ya ADF nchini DRC, alisema wanachama wengine sita wa kikosi hicho waliuawa kwa kupigwa risasi katika operesheni ya Jumanne.

Baada ya shambulio la Oktoba, rais Yoweri Museveni alitoa wito kwa vikosi vya usalama kuhakikisha ADF "ilifutwa" na jeshi limefanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya nafasi zake nchini DRC.

Mwezi Juni, wapiganaji wa ADF na kuwaua watu 42 wakiwemo wanafunzi 37 katika shambulio la shule ya sekondari Magharibi mwa Uganda karibu na mpaka wa DRC.

Utalii ni kipato cha juu cha fedha za kigeni nchini Uganda, kinachozalisha karibu asilimia 10 ya Pato la Taifa (GDP) mwaka jana, kulingana na takwimu za serikali.

AFP