Serikali ya Uganda ilianza ujenzi wa jengo hilo jipya la kisasa kuanzia Juni 2021 hadi mwisho wa Agosti 2023 na kubomoa jengo la awali.
Jengo lenyewe liko karibu na barabara pekee nchini DRC, iliyopewa jina la nchi yaani barabara ya 'Ouganda' mjini Kinshasa.
Uganda imesema kuwa barabara hiyo imeitwa hivyo tangu miaka ya 1970 na haijawahi kubadilishwa jina, hata wakati wa kurasa zenye shida za historia ya pamoja ya nchi hizo mbili.
Aidha, Uganda inasema kuwa jengo hilo jipya na la kisasa linaashiria mwanzo wa ukurasa mpya wa uwepo wa kidiplomasia wa Uganda nchini DRC.
Hivi majuzi, nchi hizo mbili ziliondoa mahitaji ya visa ya kuingia kwa raia wao.
Kupitia ujumbe wa waziri wa mambo ya nje anayesimamia masuala ya kikanda John Mulimba aliyewakilishwa katika hafla hiyo na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya Nje Norah Bigirwa Nyendwoha, alisema "Tutumie fursa hii kukuza mazungumzo, kukuza diplomasia, na kutoa suluhisho za ubunifu ambazo zinachangia utambuzi wa mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo."
Alibainisha kuwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zina historia ndefu na hatima ya kawaida.
"Sisi ni nchi mbili zilizo na utajiri wa maliasili na idadi kubwa ya watu. Nchi hizi zote mbili zinatambua umuhimu wa utulivu wa kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa faida yetu ya pande zote".
Kwa upande wake, mkuu wa ujumbe wa Uganda mjini Kinshasa, Balozi wa DRC Farid Kaliisa alisema kuwa nchi hizo mbili ziliamua kurekebisha uhusiano wao wa kidiplomasia mwaka 2007. Wakati huo jengo hilo la ubalozi wa Uganda huko Kinshasa, lilikuwa karibu kuharibika.
"Jengo hili jipya ni zaidi ya makazi mapya ya ofisi kwa Ubalozi wa Uganda. Inaashiria uhusiano wa kina na wa kudumu kati ya Uganda na DRC." Kaliisa alisema.
Ni mahali ambapo watu kutoka Uganda na DRC wanaweza kuja pamoja kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kubadilishana mawazo na kujenga ushirikiano," Kaliisa alisema.