Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema hapatokuwa na sababu yoyote ya kuchelewesha mazungumzo ya kumaliza mashambulizi dhidi ya Gaza.
"Hali inayoendelea Gaza haiwezi kusubiriwa zaidi," alisema al-Sisi katika kikao chake na Kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la Uingereza, mjini Cairo siku ya Jumatano.
Mkutano huo ulijadili hali ya usalama wa kanda hiyo, hasa katika ukanda wa Gaza, kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Misri.
Kuachia huru wafungwa
Toka Jumapili, mazungumzo yameendelea katika mji mkuu wa Misri wa Cairo, ukihusisha Misri, Marekani, Qatar na Hamas, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Serikali la nchi hiyo la Al-Qahera.
Mazungumzo mapya ya kumaliza mashambulizi ya Gaza yameanza mjini Cairo siku ya Jumapili, huku kukiwa na uwakilishi kutoka Misri, Qatar, Marekani na kikundi cha Hamas.
Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, wasulihishi wa mgogoro huo wanalenga kutatua uhasama kati ya Israel na Hamas, kwa Israel kujiondoa katika eneo la Gaza, pamoja na kuwaachia huru wafungwa kutoka pande zote.
Hamas inaaminika kuwashikilia zaidi ya mateka 130 wa Israel, toka yalipotokea mashambulizi ya Oktoba 7.
Israel imeendesha mashambulizi mfululizo dhidi ya Gaza, ambayo yamefikia siku ya 153 na kuua watu takribani 1,200.
Vizuizi vya kulemaza
Zaidi ya wapalestina 30,700 wameuwawa na zaidi ya 72,000 kujeruhiwa, huku kukiwa na uharibu mkubwa wa mali na upungufu wa mahitaji muhimu ya maisha.
Israel pia imetangaza vizuizi kwenye ukanda wa Gaza, na kuwaacha raia wa eneo hilo katika baa la njaa.
Vita hivyo vimewaacha zaidi ya asilimia 85 ya watu wa Gaza bila makazi, huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, wakati asilimia 60 ya miundombinu ikiharibiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Israel inatahukumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Maamuzi ya mpito yameitaka Tel Aviv kusitisha vitendo hivyo na kutoa uhakika wa hatua za kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wa Gaza.