George Weah amehudumu kama rais wa Liberia tangu Januari 22, 2018. / Picha: Reuters

Rais wa Liberia George Weah anakabiliwa na kura ya marudio ya Novemba 14 baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu kwa chini ya nusu ya alama katika duru ya kwanza, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisema Jumanne ikitangaza matokeo ya mwisho.

Nyota wa zamani wa soka wa kimataifa Weah alipata kura 804,087 (43.83%) kutoka uchaguzi wa Oktoba 10 huku Joseph Boakai akipata kura 796,961 (43.44%), mkuu wa tume ya uchaguzi Davidetta Browne-Lansanah alisema.

Joseph Boakai alihudumu kama makamu wa rais wa Liberia kati ya 2006 na 2018. / Picha: AA

Kwa kuwa hakuna mgombeaji anayepata kura za kutosha kwa wingi kamili wa kuchaguliwa, "kura ya marudio inatangazwa Jumanne, tarehe 14 Novemba 2023," alisema.

Hilo linaanzisha marudio ya duru ya pili ya uchaguzi wa 2017 ambayo ilimshuhudia Weah, anayependwa na vijana wengi, akitangazwa rais.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 57 amekosolewa baada ya muhula wa kwanza wa kukatisha tamaa na kushutumiwa kwa kuvunja ahadi.

Ahadi za zamani, ahadi za sasa na ahadi siku sijazo

Hali ya maisha haijaboreka kwa wengi wa watu maskini zaidi wa taifa hilo, na ufisadi umeongezeka.

Marekani imewawekea vikwazo maafisa watano wakuu wa Liberia kwa ufisadi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Boakai, mwenye umri wa miaka 78, alikuwa makamu wa rais kutoka 2006 hadi 2018 na amekuwa mtu muhimu katika siasa za kitaifa kwa karibu miongo minne.

Ameahidi kurejesha sura ya nchi, kuendeleza miundombinu na kuboresha maisha ya watu wasiojiweza.

'Tayari kwa duru ya pili'

Kabla ya matokeo ya mwisho kutolewa msemaji wa Boakai Mohammed Ali aliiambia AFP kwamba mpinzani yuko tayari kwa duru ya pili ya kampeni, licha ya dosari za upigaji kura katika duru ya kwanza kama vile kura batili kuhesabiwa na matatizo ya kutambua baadhi ya wapiga kura.

Hakuna hata mmoja wa wagombea wengine 18 wa urais alipata zaidi ya 3% katika duru ya kwanza ya upigaji kura katika taifa hilo la Afrika Magharibi mnamo Oktoba 10.

Tume ya uchaguzi ilibainisha kuwa asilimia 78.86 ya waliojitokeza kupiga kura katika duru ya kwanza ya upigaji kura ilikuwa "ya kihistoria" na "rekodi mpya".

Waangalizi wa kimataifa wamepongeza tume ya uchaguzi kwa mwenendo mzuri wa duru ya kwanza. Hakukuwa na matukio makubwa.

TRT Afrika