Uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini 2024: Fahamu vyama vinavyoshinda. Picha: Maktaba

Uchaguzi mkuu wa Mei 29 nchini Afrika Kusini huenda ukaleta mabadiliko makubwa, huku kura za maoni zikidokeza kuwa Chama tawala cha African National Congress-ANC huenda kikapoteza kura nyingi baada ya miaka 30 madarakani.

ANC - African National Congress

ANC inajivunia uaminifu thabiti kutoka kwa weusi wengi wa Afrika Kusini, haswa wapiga kura wazee, kwa sababu ya ushujaa wake wa zamani kama harakati ya ukombozi ambayo ilisaidia kutokomeza utawala wa ubaguzi wa rangi na kuanzisha demokrasia ya rangi nyingi chini ya uongozi wa Nelson Mandela.

ANC ina historia ya kupata kura nyingi katika kila uchaguzi wa kitaifa uliofanyika baada ya kila miaka mitano tangu 1994.

ANC imepata kura nyingi katika kila uchaguzi wa kitaifa unaofanyika baada ya kila miaka mitano tangu 1994. Picha: AFP

Iwapo kura za maoni ni sahihi, basi ANC iko njiani kupoteza ushawishi wake mkubwa kwa mara ya kwanza tangu ilipoingia madarakani, lakini bado inasalia kuwa chama kikubwa, na iwapo katika uchaguzi huu itashindwa kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge, basi italazimika kuingia katika mazungumzo na vyama vyengine ili kuunda serikali ya pamoja.

ANC imewakosoa wengi kwa idadi ya kura ilizopata katika uchaguzi uliopita na wachambuzi wengine wanasema kuwa inaweza kushinda tena, wakionyesha nguvu zake za kampeni ya kutisha na faida ya kuendelea kuwa madarakani.

CHAMA CHA DA - DEMOCRATIC ALLIANCE

Chama cha kutetea biashara DA, kilichopata kura ya pili kwa ukubwa katika uchaguzi uliopita, kimeungana na vyama kadhaa vidogo katika jitihada za kupanua mabawa yake.

Kiongozi wa chama cha upinzani DA John Steenhuisen. Picha: Maktaba

Chama hicho kinatawala serikali ya mkoa wa Western Cape, ambapo mji wa pili wenye idadi kubwa ya watu nchini Afrika Kusini, Cape Town, uko.

Chama hicho kinapendekeza kuondoa mpango wa ANC wa uwezeshaji wa weusi, ambao kiongozi wa DA John Steenhuisen ameshutumu kama "kuhesabu maharagwe ya rangi," kwa niaba ya sera zinazozingatia kupunguza umaskini bila kujali rangi ya ngozi.

Steenhuisen, ambaye hajapinga uwezekano wa makubaliano ya baada ya uchaguzi na ANC, amekataa ukosoaji unaodai kwamba DA inawakilisha upendeleo wa wazungu, akisema inataka kufanya utawala mzuri kwa faida ya Waafrika Kusini wote.

DA ilitoa tangazo la kampeni lililoonyesha bendera ya Afrika Kusini ikiteketea polepole, kama ishara ya hatari zinazokabili taifa ikiwa ANC itaingia katika muungano na vyama vyenye mrengo wa kushoto.

Kwa upande wake, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameilaani kama kile alichokiita matumizi mabaya ya bendera ya taifa kwa madhumuni ya kisiasa ya chama.

EFF - ECONOMIC FREEDOM FIGHTERS

Chama hiki kiliundwa mnamo 2013 na Julius Malema, kiongozi wa zamani wa tawi la vijana, ANC, kabla ya kujitenga na chama hicho.

EFF inavutia wafuasi hasa kutoka kwa wapiga kura ambao ni vijana, maskini na weusi.

Chama cha EFF kinaongozwa na Julius Malema, kiongozi wa zamani wa tawi la vijana, ANC. Picha: AFP

Chama hicho kinajiwakilisha kama 'Marxist,' kikitetea utaifishaji wa viwanda na usambazaji wa ardhi kusuluhisha ukosefu wa haki za rangi, sera ambazo hazipendwi na jamii ya wafanyabiashara wa Afrika Kusini.

EFF inaonekana kama mshirika wa muungano wa ANC kutokana na uhusiano wa kihistoria wa Malema na chama tawala - ANC.

UMKHONTO WE SIZWE - (MK)

Jina la chama hiki, MK linatokana na jina la mrengo wa zamani wenye silaha wa ANC katika enzi za ubaguzi wa rangi.

Chama hiki cha MK, ingawa kimejitosa ulingoni hivi karibuni, baada ya kusajiliwa Septemba 2023, lakini kilipata msukumo mkubwa wakati rais wa zamani Jacob Zuma, ambaye ametengana na ANC, alitangaza mnamo Disemba kwamba anakiunga mkono.

Jina la chama hiki, MK linatokana na jina la mrengo wa zamani wenye silaha wa ANC katika enzi za ubaguzi wa rangi. Picha; AFP

Uchunguzi unaonyesha kuwa imekuwa ikifyonza ngome ya EFF na inaweza kuvutia kura kubwa mnamo Mei 29, haswa katika jimbo la nyumbani la Zuma la KwaZulu Natal ambapo anaendelea kuwa na wafuasi waaminifu.

Malema wa EFF ambaye ana historia ya kutofautiana na Zuma, amesema chama chake kiko tayari muungano baada ya uchaguzi na MK.

Hapo zamani, Malema alikuwa mfuasi wa Zuma, lakini wawili hao walitofautiana, na baada ya hapo, Malema aliondoka ANC.

IFP - INKATHA FREEDOM PARTY

IFP ya kihafidhina ya kijamii, inayoongozwa na Velenkosini Hlabisa, inaungwa mkono na mkoa wa KwaZulu Natal, eneo la Zulu.

Sera zake zinatilia mkazo kuwapa watawala wa kitamaduni mamlaka zaidi na kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu kurudisha adhabu ya kifo.

Kilianzishwa mnamo 1975 na kiongozi wa kitaifa wa Zulu Mangosuthu Buthelezi, IFP na kina historia iliyojaa ya ANC. Vyama hivi vilikuwa katika migogoro ya vurugu wakati wa miaka ya mwisho ya ubaguzi wa rangi, lakini vilishirikiana katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa baada ya uchaguzi wa 1994.

ACTIONSA

Chama hiki kilichoanzishwa mnamo 2020, ni maarufu katika mkoa tajiri zaidi wa Gauteng, wenye mji wa kibiashara wa Johannesburg. Kiongozi wake ni Herman Mashaba, meya wa zamani wa jiji hilo, ingawa alikuwa sehemu ya DA wakati huo.

Reuters