Wachezaji wa handiboli wa Burundi Waliotoweka nchini Croatia mwezi jana wamepatikana nchini Ubelgiji wakiomba hifadhi nchini humo.
Burundi ilishiriki Katika Kombe la Dunia la Handiboli la U19 (Agosti) huko Croatia. Hata hivyo wachezaji kumi kutoka timu ya taifa ya Burundi walitoweka kikosini.
Waziri wa Ubelgiji wa mambo ya nje, hifadhi na uhamiaji, Nicole de Moor, amesema kuwa baadhi ya wanariadha chipukizi ambao walikuwa wametoweka agosti 9 Huko Rijeka, mji Wa Croatia, walikuwa wamewasilisha maombi yao ya hifadhi nchini Ubelgiji.
"Kwa sasa ofisi zetu zinawasiliana na Croatia kuandaa kurudi kwao, na hilo litawezekana tu ikiwa wana umri unaofaa kisheria. Usafiri bandia wa wanaotafuta hifadhi kwa nchi mbalimbali za ulaya ndio hasa kasoro iliyoko kwenye sera ya hifadhi ya Ulaya, " de Moor alisema kuhusu suala hilo.
Ingawa waziri huyo hakutaja idadi kamili ya walioomba hifadhi kutoka kundi hilo, shirika la habari la Ubelgiji limefichua kwamba ni 'sehemu kubwa ya timu hiyo'.
Ubelgiji, wakoloni wa zamani wa Burundi, inawapokea jamii kubwa ya raia wa Burundi.
Kwa upande mwingine, Waziri de Moor amesema kuwa wale ambao wameomba hifadhi wanakaribishwa kufanya hivyo lakini wanariadha wa Burundi ni jukumu la Croatia, kwani inachukuliwa kuwa wamefaidika na visa ya kuishi kwa muda mfupi kushiriki mashindano hayo, kabla ya kuomba hifadhi katika Nchi nyingine ya Schengen.
Mwezi uliopita, polisi nchini Croatia walibainisha kuwa vijana kumi, "waliozaliwa mwaka 2006", walikuwa wameacha maeneo yao ya malazi katika makazi ya chuo kikuu mjini Rijeka.
Polisi hao waliongeza kuwa wachezaji kumi wa mpira wa mikono walikuwa wamefika katika nchi hiyo ya Ulay kushiriki mashindano ya dunia ya vijana.
Mwezi jana, Rais wa Shirikisho la handiboli Burundi alinukuliwa na vyombo vya habari vya croatia akielezea hasira na wasiwasi wake juu ya kutoweka kwa wachezaji hao.
"Kama shirikisho na wazazi wa wachezaji wetu wa timu ya taifa tumeshtuka. Tunaomba mtu yeyote ambaye anaweza kutusaidia kuwapata wavulana wetu kufanya hivyo. Sijui hata tutafikaje nyumbani bila wao," alisema.
Lakini hatma ya vijana hao kuhusu iwapo watapata sehemu ya hifadhi bado haijajulikana kwani makazi ambayo hutolewa kwa wakimbizi wa kimataifa nchini Ubelgiji, imekumbwa na msongamano baada ya ya Ubelgiji kutangaza kuwakataa wanaume ambao hawanajoa kupisha nafasi kwa wale wenye familia na watoto.