Walinzi wa Pwani wa Tunisia wanasema kuwa wameokoa miili tisa ya wahamiaji wa kiafrika na kuokoa 29 wengine, baada ya mashua yao kuzama kwenye pwani ya Monastir walipokuwa wakijaribu kufika pwani ya Italia.
Kazi ya kuwaokoa watu inaendelea ikiwasaka watu waliokufa kwa kuzama katika janga hili jipya katika pwani ya Tunisia, anasema msemaji Farid Ben Jaha.
Mapema wiki hii, walinzi wa pwani walitangaza wahamiaji 29 kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wamepatikana baada ya meli tatu kupinduka.
Operesheni pia "iliokoa wahamiaji haramu 11 wa mataifa mbalimbali ya Afrika baada ya boti zao kuzama" katika pwani ya kati-mashariki, ilisema katika taarifa yake, ikitaja matukio matatu tofauti ya kuzama kwa boti.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema watu wengi hufa kila baada ya siku kumi katika vivuko hatari katika ufukwe wa Afrika Kaskazini.
Watu wanaokimbia umaskini na ghasia katika jimbo la Darfur nchini Sudan, Afrika Magharibi, na maeneo mengine ya bara hilo kwa miaka mingi wametumia Tunisia kama njia ya majaribio ya hatari ya kufikia usalama na maisha bora barani Ulaya.
Mradi wa wahamiaji waliopotea unaojulikana kama 'the Missing Migrants Project' unasema zaidi ya wahamiaji 12,000 wamekufa au hawajulikani waliko tangu 2014.