Tetemeko la ardhi la kipimo cha 4.9 lilipiga eneo karibu na mpaka kati ya Sudan Kusini na Uganda siku ya Jumatatu, Kituo cha Ulaya cha kufuatilia shughuli na mitikisiko ya ardhi duniani (EMSC) kilisema.
Hata hivyo tetemeko hilo lilikuwa umbali wa kilomita nane ndani ya radhi.
Hakuna madhara yaliyoripotiw akutokana na tetemeko hilo la Jumatatu usiku.
Taarifa za mitandao ya kijamii zinasema kuwa tetemeko hilo lilisikika katika sehemu za mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, ndani ya Uganda na kulikotokea kitovu chake Kusini mwa Sudan Kusini.
''Ni mara yangu ya kwanza kukumbana na tetemeko la ardhi kama hilo la mpigo wa moyo ambalo lilitokea kwenye mpaka kati ya Sudan Kusini na Uganda ambayo ni takriban Km 35.2 kutoka wilaya ya Nyumbani kwangu ya Yumbe. Mwanzoni nilidhani lori kubwa linakuja lakini nilipata vibrating yangu pia.'' anasema @AgatareAlex katika mtandao wa X.
Kwa mujibu wa shirka hilo la kuchunguza mitetemeko, EMSC, eneo hilo limerekodi mitetemeko midogo mara kwa mara katika vipimo vya wastani vya 4 au chini vya Richter.
Mnamo Februari 6, 1994, tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.5 lilipiga wilaya ya Kabarole na kuua watu wanane na kuharibu majengo mengi. Kitovu hicho kilikuwa katika Kaunti Ndogo ya Kisomoro.
Tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi lililorekodiwa nchini Uganda lilitokea Machi 20, 1966 huko Tooro na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 157.