Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Tanzania, Jenerali Musuguri./Picha: Wengine

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali David Musuguri, amefariki dunia.

Jenerali Musuguri, aliyekuwa na umri wa miaka 104, alifariki dunia Oktoba 29,2024 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, nchini Tanzania, alipokuwa anapatiwa matibabu, familia yake imethibitisha.

Jenerali huyo mstaafu, alihudumu nafasi hiyo kuanzia mwaka 1980 hadi 1988.

Atakumbukwa kwa kuiongoza JWTZ kuukomboa mji wa Kagera nchini Tanzania, wakati kiongozi wa zamani wa Uganda Idi Amin, alipovamia eneo hilo Oktoba 1978.

Vita hivyo vilitokana na uvamizi alioufanya Iddi yo ilitokana na uvamizi alioufanya Idi Amin katika mkoa wa Kagera, jambo ambalo lilimchukiza Rais wa Tanzania wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere, huku akiamuru vikosi vya Tanzania kuchukua hatua.

Mbali na vita vya Kagera, Jenerali Musuguri pia alishiriki katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, na Battle of Simba Hills.

TRT Afrika