Mvua kubw ailiyonyesha ilisababisha mgodi huo kuporomoka na kuwazika waathiriwa. Awali watu hao walikaidi amri ya kutingia mgodini / Picha reuters 

Kuporomoka kwa mgodi mdogo wa dhahabu haramu kumesababisha vifo vya takriban watu 22 kaskazini mwa Tanzania kufuatia mvua kubwa iliyonyesha, afisa mkuu wa serikali alisema Jumapili.

Ajali hiyo ilitokea mapema Jumamosi mkoani Simiyu baada ya kundi la watu wenye umri wa kati ya miaka 24 na 38 kuanza uchimbaji wa madini katika eneo ambalo shughuli ilikuwa imezuiwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani humo, Simon Simalenga, aliliambia shirika la habari la Reuters.

“Awali tuliambiwa kuna watu 19 hadi 20 ambao wamenasa migodini lakini kwa bahati mbaya tukaishia kuopoa miili 22,” alisema na kuongeza kuwa zoezi la kuwasaka na kuwaokoa linaendelea japo karibu vifusi vyote vilivyokuwa vimewafukia sasa imeondolewa.

Simalenga alisema kikundi hicho kiligundua eneo lenye madini mengi takribani wiki mbili hadi tatu zilizopita na kuhamia kuanza uchimbaji kabla ya serikali kuidhinisha usalama na taratibu za kimazingira.

“Ofisa madini wa mkoa aliwatembelea na kuwazuia kuchimba madini kwa kuwa ilikuwa inafanyia kazi taratibu zinazotakiwa,” alisema.

Kundi hilo lilikaidi agizo hilo, aliongeza, lilianza kuchimba madini siku ya Ijumaa kabla ya sehemu ya eneo hilo kuzama na kuwazika ndani.

Serikali imefanya kazi kwa miaka mingi kuimarisha usalama kwa wachimbaji wadogo lakini uchimbaji haramu usio salama na usiodhibitiwa bado unaendelea nchini Tanzania, ambayo ni nchi ya nne barani Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali.

Reuters