Chama cha upinzani nchini Burundi National Freedom Council (CNL),  Agathon Rwasa akiwahutubia wafuasi wake wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo la Ngozi, Burundi Aprili 27, 2020. REUTERS/Evrard Ngendakumana

Baada ya kutangazwa kwa kusimamishwa kwake, CNL ilishutumu uamuzi "usio wa kikatiba" na nia ya serikali kuzuia njia yao kwa uchaguzi ujao.

Serikali ya Burundi kupitia msemaji wao Prosper Ntahorwamiye, wameiambia TRT Afrika leo tarehe 8 Juni kuwa ni suala la "subiri uone" kuhusu madai ya CNL juu yao.

Katibu mkuu wa chama cha Baraza la Uhuru la Kitaifa, CNL, Simon Bizimungu, aliiambia AFP kuwa uamuzi huo ni "ukiukwaji mkubwa wa katiba" na kwamba ni "jaribio la kuifanya CNL kuwa dhaifu kabla ya uchaguzi wa bunge wa 2025".

Hatua hiyo iliyotangazwa na wizara ya mambo ya ndani, katika barua iliyotolewa Jumanne, inaweza kuzidisha vurugu za kisiasa zilizolikumba taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Kujibu hatua hiyo, CNL, lilitangaza "ukiukwaji mkubwa wa katiba" katika jaribio la "kuihujumu na kuifanya chama kuwa dhaifu" baada ya mipaka mpya ya uchaguzi kuanza kutumika mwaka 2025.

AFP imeripoti kuwa, Wizara ilisema ilikuwa inajibu malalamiko ya viongozi nane wa CNL ambao walitimuliwa baada ya kupinga rais wa chama, Agathon Rwasa, katika mikutano miwili ya hivi karibuni ya chama.

"Shughuli zote zinazofanywa na makundi yaliyoanzishwa kinyume cha taratibu zimesimamishwa nchi nzima," ilisema.

"Mikutano pekee inayolenga kupunguza mivutano ndani ya chama ndiyo inayoruhusiwa," ilisema.

"Hakuna mivutano au upinzani ndani ya chama. Ni suala tu la wapinzani wanane ambao hawana ushawishi wowote, lakini wanaungwa mkono na mamlaka za umma," alisema.

TRT Afrika na mashirika ya habari