Mapambo ya shanga yanahusishwa na kabila la Maasai linalopatikana kaskazini, kati na kusini mwa Kenya na kaskazini mwa Tanzania. Nchini Kenya, wanawake wengi wanapendelea mapambo yenye urembo wa kimaasai.
Mapambo ya shanga huuzwa kuanzia dola mbili had dola 60 hasa kwa zile shanga kubwa ambazo huchukua muda mrefu kutengenezwa.
Wateja nao wanasema wanapenda kuja sokoni kwa sababu mapambo tofauti yanapatikana sehemu moja.
Wengine wanasema wao huja kununua mapambo pindi wanaposafiri kwenda nchi za Ulaya ili wajivunie kuwa na mapambo yenye asili ya kiafrika.
Wafanyabiashara wengine hutengeza mapambo yatokanayo na shaba na pembe za ng'ombe.
Nguo zinazotengenezwa nchini Kenya, baadhi zina lengo la kuendeleza tamaduni za kiafrika. Baadhi ya wanunuzi huzinunua kwa wingi kwa ajili ya kuziuza nchi za Ulaya.
Soko hili limekuwa nafasi mwafaka kwa raia wa Kenya na wageni kutafuta bidhaa asili za kiafrika.
Watengezaji wa kazi za mikono wanajitahidi kubuni miundo mipya kila siku ili kupambana na ushindani uliopo sokoni.