Katika Shughuli hiyo, makala maalumu tano zimeonyeshwa, zikiwa na vichwa kama "Kukaliwa kwa Kidijitali," "Uzayuni: Kuzalisha Taifa," "Rafah: Eneo lisilo salama," "Manusura Pekee," na "Shahidi." Kwa kuongeza, video za makala maalumu za baadae zimeonyeshwa. 

Shirika la Taifa la Utangazaji la Uturuki, Redio ya Uturuki na Televisheni (TRT), limeandaa shughuli iliyolenga Palestina na mapambano wanayokabiliana nayo watu wa Palestina katikati ya mashambulizi ya Israeli.

Katika shughuli hiyo ya "Usiku wa Palestina Ramadhan" iliyofanyika katika kampasi ya TRT Ulus mjini Istanbul, Mkurugenzi Mkuu wa TRT, Mehmet Zahid Sobaci, ametoa kauli zenye hisia kali siku ya Ijumaa. Amesema, "Hivi karibuni, Israeli itabaini kwamba haiwezi kuishi kupitia damu za watoto wasio na hatia."

"Tunapofunga Ramadhan, mioyo yetu iko pamoja na kaka zetu na dada zetu wanaopitia mateso makubwa," amesema Sobaci. "Leo, tunasimama kuonyesha mshikamano pamoja na wale waliopo Gaza, Rafah, na West Bank, kuthibitisha kwamba hawapo pekee yao katika mapambano."

Sobaci pia amekosoa dhana hasi ambao mara nyingi huonyeshwa na vyombo vya habari vya magharibi. "Licha ya utoposhaji wa vyombo vya habari vya Magharibi, tunabaki madhubuti katika kuonyesha ukweli kamili. Jitihada za IsraelI za kuficha vitendo vyake, haviwezi kuficha mauaji yanayoonekana mbele ya dunia. Mauaji ya halaiki wanayojaribu kuyaficha yanaonekana dhahiri."

"Hali hii inaonyesha ukosefu wa maadili katika jamii ya magharibi, ambayo inadai kusimamia maadili ya dunia lakini mara nyingi inashindwa kuyatekeleza," ameongeza.

"Tumeshuhudiwa namna gani mtizamo wa uhuru wa kujieleza mara kadhaa unavyotumiwa vibaya na Magharibi. Uhuru wa kujieleza wa kweli unatakiwa kuvuka mipaka ya tamaduni na kutekelezwa kote," amesema Sobaci.

'Uharibifu uliozidi asilimia 70 Gaza'

Akizungumza katika shughuli hiyo, iliyoandaliwa na TRT, Balozi wa Palestina Uturuki, Dk. Faed Mustafa, amerudia kauli ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan "Dunia ni kubwa zaidi ya watano" na kusema, "Mfumo wa sasa wa kimataifa haukuwaokoa Wapalestina na haukutimiza haki."

“Dhulma itaisha pindi Wapalestina watakapoweza kuunda taifa huru la Palestina na Jerusalem kuwa mji mkuu,” balozi amesema.

"Tunazungumzia uharibufu wa zaidi ya asilimia 70 ya ardhi ya Gaza. Uharibifu ulioharibu kila kitu Gaza, ikiwemo hospitali, vyuo vikuu, shule, misikiti, na makanisa. Hawajaacha kitu Gaza," amesema Mustafa.

"Ni kweli kwamba, sisi Wapalestina tumekabiliana na miezi sita ya taabu. Hata hivyo, dhulma haikuanza Oktoba 7."

Katika Shughuli hiyo, makala maalumu tano zimeonyeshwa, zikiwa na vichwa kama "Kukaliwa kwa Kidijitali," "Uzayuni: Kuzalisha Taifa," "Rafah: Eneo lisilo salama," "Manusura Pekee," na "Shahidi." Kwa kuongeza, video za makala maalumu za baadae zimeonyeshwa.

Makala hizo maalumu zimeangazia aina mbalimbali ya mgogoro wa Israeli-Palestina.

Mashambulizi mabaya ya kijeshi

Israeli imefanya mashambulizi ya kijeshi mabaya zaidi Gaza tangu shambulizi za kuvuka mpaka lililofanywa na Hamas Oktoba 7.

Takriban Wapalestina 32,000, wengi wao wanawake na watoto, wameuawa Gaza, na zaidi ya 74,000 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa bidhaa muhimu.

Mashambulizi ya Israeli yamesukuma asilimia 85 ya idadi ya wakazi wa Gaza kuwa wakimbizi wa ndani huku chakula, maji safi na dawa zikizuiwa, na asilimia 60 ya miundombinu kuharibiwa, kwa mujibu wa UN.

TRT World