Maiti zaendele kufukuliwa aktika msitu wa shakahola mjini Malindi Kenya. Picha : Twitter Waziri, @KithureKindiki

Makundi ya uokoaji yamefukua maiti 22 zaidi Jumamosi na kufikisha idadi kamili ya maiti zilizo patikana katika msitu wa Shakahola 201.

Kwa mujibu wa kamishna wa polisi wa mkoa wa pwani, Rhoda Onyancha, watu 26 wamekamatwa, wanaoshukiwa kuwa katika kundi lilitumika ‘kuhakikisha hakuna anayevunja mfungo wake’ ambapo waumini walitakiwa kukosa kula na kunywa hadi kufa ili wakutane na Yesu.

Onyancha aliongeza kuwa polisi watasitisha kwa muda wa siku mbili shughuli ya kutafuta maiti Ili kurejelea utendaji kazi wao na mpango mpya wa kutumia.

‘‘Bado uchunguzi utaendelea, tutazidi kutafuta maiti zaidi kuanzia Jumanne. Tumeshapokea ripoti za zaidi ya watu 600 kuwa hawajilikani waliko na tutaendelea kuwatafuta,’’aliongeza Onyancha.

Idara ya upelelezi Kenya, yaendelea na uchugnuzi juu ya mauaji ya tu katika msitu wa Shakahola. Picha : Twitter Waziri wa Usalama wa ndani @KithureKindiki

Miongoni mwa wanaozuiliwa ni mwanzilishi wa kanisa la Good News International Church, Paul Nthenge Mackenzie, ambaye wiki iliyopita, mahakama iliamuru aendelee kuzuiliwa bila dhamana ili kuruhusu uchunguzi kuendelea wa kile kilichojulikana kama ‘Mauaji ya Shakahola.’

Tangu shughuli ya kufukua maiti katika msitu huo ilipoanza, imebainika kuwa wengi wao walifariki kutokana na kukosa kula na kunywa, japo mwana patholojia wa serikali amesema kuwa alikuta baadhi yao walifariki kutokana na kunyongwa, kupigwa au kuzibwa pumzi.

TRT Afrika