Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) hii leo wameidhinisha kutumwa kikosi cha kulinda amani kama mchango wao katika kutafutia suluhu mzozo wa Jamahuri ya Demokrasia ya Kongo, DRC
Viongozi hao waliokutana mjini Windhoek Namibia, pamoja na mashirika ya Organ Troika, na nchi zinazo changia vikosi vya Jeshi katika jumuiya hiyo walielezea wasiwasi wao juu ya kudorora kwa usalama mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Pia walikemea kuendelea kuzuka kwa makundi yaliyo jihami ikiwemo waasi wa M23 nchini DRC,
Jumuiya hiyo kutoka Kusini mwa Afrika wametaka kusitishwa mapigano mara moja huku wakitaka kujiondoa kwa wapiganaji hao kutoka kwenye maeneo walioteka nchini humo.
Kundi hilo pia limeitaka serikali ya DRC kuweka mikakati itakayowezesha ushirikiano wa vikosi vyote kutoka maeneo mbali mbali na mashirika ya amani yaliyomo nchini humo.
Viongozi 7 kutoka nchi wanachama wa SADC walikuwepo