Idara ya Huduma za Urekebishaji nchini Rwanda (RCS) imewafuta kazi maofisa 411 kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Kati ya waliofukuzwa ni pamoja na kamishna mmoja na maofisa waandamizi 26.
Pia wapo maofisa wa ngazi ya nchini 20 na maofisa magereza 364.
“Uamuzi wa kuwafukuza kazi maofisa hao ni kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza ufanyaji kazi wa kila siku ndani ya RCS,” idara hiyo ilisema.
Kwa mujibu wa RCS, uamuzi huo uliidhinishwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokaa siku ya Novemba 9.
TRT Afrika