Rwanda government respects the courts but disappointed

Serikali ya Rwanda imesema kuwa itaheshimu uamuzi wa mahakama kuwa itasitisha keshi inayomkabili mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Felicien Kabuga.

Rwanda hata hivyo imeelezea kusikitishwa na uamuzi huo ikisema kuwa ni pigo kwa waathiriwa wa mauaji hayo wambao wamekuwa wakisubiri kutendewa haki.

"Rwanda inaheshimu uamuzi wa mahakama ya rufaa kusimamisha kwa muda usiojulikana kesi ya Félicien Kabuga,'' msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo ameambia TRT Afrika. ''Lakini jambo hili bila shaka ni la kukatisha tamaa kwa waathiriwa na walionusurika katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi," aliongeza.

Mahakama ya rufaa ya Umoja wa Mataifa Jumatatu iliamuru kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda Felicien Kabuga isitishwe kwa muda usiojulikana kutokana na kile kimetajwa kuwa maradhi ya akili.

Mahakama ya rufaa ya UN iliamuru baraza la chini la kesi hiyo kutathmini mazingira ya kuachiliwa kwa Kabuga / Picha AFP

Mahakama hiyo, ambayo ni sehemu ya mahakama iliyofuata mahakama ya uhalifu wa kivita ya Rwanda, pia iliamuru baraza la chini la kesi hiyo kutathmini ni katika mazingira gani Kabuga anaweza kuachiliwa.

Kabuga anaaminiwa kukaribia miaka tisini ingawa tarehe yake kamili ya kuzaliwa inabishaniwa. Alikamatwa nchini Ufaransa mnamo 2020 baada ya zaidi ya miaka 20 kukimbia na kuishi mafichoni.

Majaji wa mahakam hiyo pia walitupilia mbali pendekezo la kutafuta utaratibu mbadala wa kuendelea na kesi ila kwa kumpunguzia uzito kuotkana na umri yake.

Mfanyabiashara huyo wa zamani na mmiliki wa kituo cha redio alikuwa mmoja wa washukiwa wa mwisho waliotafutwa na mahakama hiyo wakiendesha mashtaka ya uhalifu katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, wakati Wahutu wenye itikadi kali waliwauwa zaidi ya Watutsi 800,000 walio wachache na Wahutu wenye msimamo wa wastani ndani ya siku 100.

Reuters