Rwanda kuajiri mameneja fedha kwenye shule za msingi

Rwanda kuajiri mameneja fedha kwenye shule za msingi

Hatua hiyo inalenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kujisimamia kiuchumi.
Waziri wa Elimu wa Rwanda, Gaspard Twagirayezu./Picha: NESA Rwanda                           

Wizara ya Elimu nchini Rwanda imeanza mchakato wa kuajiri mameneja fedha kwenye shule za msingi za umma, hatua inayolenga kuziwezesha taasisi hizo za elimu kujisimamia kiuchumi.

Hadi kufikia sasa, jumla ya watu 466 wameshaajiriwa, Waziri wa Elimu wa Rwanda, Gaspard Twagirayezu amesema.

“Kuajiri watu wa aina hiyo kutaongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kiuchumi kwenye shule zetu za msingi,” ameeleza.

Kabla ya kufikia maamuzi hayo, shule nyingi za msingi nchini Rwanda zilitumia wakuu wa shule Nchini Rwanda, shule nyingi za msingi ziliwapatumia wakuu wao kushugulikia masuala ya kiuchumi.

Rwanda ina jumla ya shule za msingi 3,932, huku 1,326 zikiwa ni za umma.

Katika mwaka wa fedha 2020/2021, serikali ya Rwanda iliamua kupanua mradi wa lishe mashuleni, hasa kwa shule za msingi baada kuwa inafanya hivyo katika shule za sekondari.

TRT Afrika