Ripoti hiyo iitwayo "On the Trail of African Gold" ilisema siku ya Ijumaa kuwa takribani tani 435 za dhahabu zilitoroshwa nje ya bara la Afrika mwaka 2022, na hivyo kulisababishia bara hilo upotevu mkubwa wa mapato kutokana na rushwa na migogoro yenye kuhusisha silaha.
Kulingana na ripoti hiyo, Uswisi, Umoja wa Falme za Kiarabu na India ndio nchi zinazoongoza kwa mauzo ya dhahabu ya Kiafrika.
Mali, Zimbabwe na Ivory Coast ndio zenye kuongoza kwa uzalishwaji wa dhahabu barani Afrika.
Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Uswisi imedokeza kuwa Afrika huzalisha kati ya tani 321 hadi 474 ya dhahabu isiyosajiliwa kila mwaka.
Iliongeza kuwa uturoshwaji wa madini hayo uliongezeka mara mbili kwa mwaka 2022, ukilinganishwa na miaka ya nyuma.
Nchi zenye kiwango kingi cha dhahabu isiyosajiliwa kulingana na ripoti hiyo ni pamoja na Ghana, Afrika Kusini, Guinea na Burkina Faso.
Mbali na hayo, ripoti hiyo ilibainisha kuwa kiasi cha dhahabu kilichochimbwa na ambacho hakijasajiliwa barani Afrika ni kikubwa kuliko ilivyokadiriwa.