Chama tawala cha ANC kitalazimika kutengeneza muungano na vyama vingine baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Mei 29, 2024. / Picha: AFP  

Rais Cyril Ramaphosa amewataka viongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya umma baada ya chama chake cha ANC kupoteza kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa zamani Jacob Zuma kususia sherehe za matokeo na chama chake kilikataa kutambua matokeo.

Hesabu za mwisho zimekipa chama tawala cha ANC nafasi 159 katika Bunge lenye viti 400, alama zake za chini zaidi katika uchaguzi mkuu.

Chama cha upinzani cha mrengo wa kati cha Democratic Alliance (DA) kilipata kura 87, uMkhonto weSizwe (MK) cha Zuma kikipata 58 na Economic Freedom Fighters (EFF) cha Julius Malema kuambulia kura 39.

Serikali ya Muungano

Chama hicho cha ukombozi wa Afrika Kusini kimepoteza asilimia 40 ya kura kutoka 57 ilizopata mwaka 2019.

Bunge jipya linategemewa kukutana ndani ya wiki mbili na kazi yake ya kwanza itakuwa ni kumchagua rais wa kuunda serikali mpya.

Lakini, bila kuwa na mshindi wa moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu kupatikana kwa demokrasia nchini humo, ANC itahitaji uungwaji mkono kutoka nje ili kufanikisha kuchaguliwa tena kwa Ramaphosa.

Katika risala yake ya Jumapili, Ramaphosa alionekana kukubaliana na mpango huo, lakini akasisitiza kwa pande zote kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

'Watu wazungumza'

"Tutake tusitake, watu wetu wamezungumza," amesema Ramaphosa.

"Kama viongozi wa vyama vya siasa...ni vyema tuheshimu matakwa yao."

Kiongozi wa chama cha DA, John Steenhuisen ameonesha nia ya kufanya kazi na ANC.

Alielezea ahadi katika ilani za MK na EFF za kutaifisha ardhi inayomilikiwa na watu binafsi na kudhoofisha uhuru wa mahakama kama "mashambulizi ya kila namna kwa katiba ya nchi yetu."

'ANC yazungumza na kila mtu'

Katibu Mkuu wa ANC Fikile Mbalula aliiambia AFP kuwa chama chake "kipo kwenye mazungumzo ya haraka ili kutekeleza mpango huo."

Kama ishara ya mgawanyiko kwa siku zijazo, wafuasi wa Zuma katika jimbo la mashariki la KwaZulu-Natal waliandamana mashambani kusherehekea yenye kelele lakini walisusia kutangazwa kwa matokeo ya mkoa huko Durban na hafla ya kitaifa huko Johannesburg.

Alipoulizwa kwa nini Zuma alikaa mbali, msemaji wa MK Nhlamulo Ndhlela alisema kuhudhuria itakuwa "sawa na kuidhinisha tamko lisilo halali."

Siku ya Jumamosi, Zuma alionya kuwa kuseka kuwa hakurididhwa na matokeo kutakuwa sawa na "uchochezi."

Wafuasi wa MK wakataa muungano

Marekani haikuonekana kuwa na wasiwasi na matokeo hayo, huku msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller akichapisha kwenye mitandao ya kijamii kuwapongeza Waafrika Kusini kwa "kuhudumu kama mshika viwango vya demokrasia barani Afrika na duniani kote."

Chama cha MK cha Jacob Zuma, kilichoanzishwa miezi nane ijayo, kiliongoza kwa kura katika jimbo la KwaZulu-Natal.

Wafuasi wake wamesema hawatajiunga na muungano isipokuwa kuwe na makubaliano ya kumsamehe Zuma kwa hukumu ambayo ilimwona akipigwa marufuku kuwa mgombea ubunge, na kuandika upya katiba ili kumruhusu kugombea.

Zuma, aliondolewa madarakani na kunyang'anywa nafasi ya uongozi wa ANC mwaka 2018 kufuatia tuhuma za ufisadi, na alifungwa ka kudharau mahakama mwaka 2021, hali iliyoibua vurugu kubwa zilizosababisha mauaji ya watu 350.

Wito wa utulivu

Waziri anayeshughulikia masuala ya polisi nchini humo, Bheki Cele alisema vikosi vya usalama viko tayari "kuhakikisha hali ya amani inaendelea baada ya uchaguzi."

Akizungumza pamoja naye, Waziri wa Ulinzi Thandi Modise alisema serikali "haijashirikiana moja kwa moja na chama cha MK" lakini "ilitoa wito wa utulivu wakati wa kampeni."

"Hatutomvumilia mtu yeyote atakayekuwa tayari kuchafua taswira ya Afrika Kusini," alisema Modise.

Chama cha ANC kimejipatia heshima miongoni mwa raia wa Afrika Kusini kufuatia kuondoa madarakani utawala wa kibaguzi wa wazungi wachache.

Hali ya kijamii

Sera zake zinazoendelea za ustawi wa jamii na uwezeshaji watu weusi kiuchumi zinapewa sifa na wafuasi kwa kusaidia mamilioni ya familia nyeusi kutoka katika umaskini.

Lakini kwa zaidi ya miongo mitatu ya utawala ambao haujapingwa, uongozi wake umehusishwa katika msururu wa kashfa za ufisadi, huku uchumi wa bara hilo ulioendelea zaidi kiviwanda ukidorora na takwimu za uhalifu na ukosefu wa ajira zimefikia kiwango cha juu.

Reuters