#MEC82 : Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini / Picha: AFP

Mahakama ya Uchaguzi nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne iliamua kwamba rais wa zamani Jacob Zuma anaweza kugombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi ujao, ikibatilisha uamuzi wa awali uliomzuia kushiriki kwenye uchaguzi.

Uamuzi huo unamwezesha Zuma kugombea urais kwa niaba ya Chama cha uMkhonto weSizwe, chama kipya cha kisiasa alichokiunga mwaka jana baada ya kukikosoa chama tawala cha African National Congress (ANC) ambacho aliwahi kuongoza.

Tume Huru ya Uchaguzi ilikuwa imeamua awali kwamba Zuma hawezi kugombea nafasi ya uongozi kwa sababu ya historia yake ya uhalifu, baada ya kupokea pingamizi dhidi ya uteuzi wake.

Katiba ya Afrika Kusini haimruhusu mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 gerezani bila chaguo la faini kugombea nafasi ya mbunge.

AFP