Rais wa Somalia ahimiza utekelezaji wa haraka kupambana na ufisadi

Rais wa Somalia ahimiza utekelezaji wa haraka kupambana na ufisadi

Baraza la Mawaziri Somalia limepitisha maagizo mapya ya kupambana na ufisadi
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud asema kutotimiza maagizo mapya ya kukumbana na ufisadi kutasababisha adhabu ya kisheria. / Photo: AFP

Serikali ya Somalia imeanza kile inachokiita hatua kuu ya uwajibikaji nchini Somalia dhidi ya ufisadi.

"Somalia ipo wakati muhimu tunapozidisha juhudi za ujenzi wa serikali na maendeleo ya kiuchumi," rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Somalia.

"Katika kufikia mafanikio katika juhudi hizi ni muhimu kuhakikisha mifumo ya serikali inajengwa juu ya kanuni nzuri za uwajibikaji uwazi na uadilifu kwa kuzingatia sheria za nchi.”

Maagizo mpya yaliyopitishwa na baraza la mawaziri wa Somalia yataimarisha michakato ya ununuzi, upataji, usimamizi wa mali za umma na mifumo ya ukaguzi.

Rais wa Somalia amesema kukabiliana na ufisadi sio tu muhimu kimaadili lakini pia ni hitaji la awali kwa maendeleo endelevu kwa nchi ya Somalia, na kujenga Somalia yenye haki na usawa.

Rais Mohamud ameonya kuwa kutotimiza maagizo haya mapya yatasababisha adhabu ya kisheria.

TRT Afrika