Taarifa zinasema  mshambuliaji huyo ni polisi wa zamani katika miaka yake ya 20/ Picha :Reyters 

Rais wa Comoro Azali Assoumani alijeruhiwa kidogo katika shambulio la kisu siku ya Ijumaa, msemaji wa serikali ya taifa hilo la visiwa alisema, na kuongeza kuwa mshambuliaji ametiwa mbaroni.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 2 usiku. (1100 GMT) huko Salimani Itsandra, mji ulio kaskazini mwa mji mkuu Moroni, chanzo cha ndani kiliiambia Reuters.

"Rais Azali Assoumani alijeruhiwa kidogo kwa kisu wakati wa mazishi ya Sheikh mkuu wa nchi. Majeraha yake si makubwa na amerejea nyumbani," msemaji wa serikali Fatima Ahamada aliambia Reuters.

Sababu ya shambulio hilo haikufahamika mara moja.

Chanzo kutoka mji wa Salimani Itsandra kiliongeza kuwa mshambuliaji huyo ni polisi wa zamani katika miaka yake ya 20.

Mwezi Mei, Assoumani aliapishwa kwa muhula wa nne madarakani kufuatia uchaguzi wa Januari ambao wapinzani wake wanadai uligubikwa na udanganyifu wa wapiga kura.

Reuters