Profesa Mohamed Janabi./Picha: Wengine

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtangaza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa Mohamed Janabi kugombea nafasi ya ukuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kanda ya Afrika.

“Ngoja niwape siri siku ya leo. Tumepitia sifa za wenzako watano na tukaona kuwa kuwa jina lako linafaa kupelekwa WHO kw ajili ya kushindania nafasi hiyo. Kwahiyo tunajiandaa kwa hilo na wakati ukifika, tutapeleka jina lako WHO, na ni vizuri ukajiweka tayari kuanzia sasa,” alisema Rais Samia wakati akiwaapisha viongozi hao katika ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

Profesa Mohamed Janabi atawania nafasi ya mkuu wa WHO kwa kanda ya Afrika kufuatia kifo cha Dkt Faustine Ndugulile kilichotokea Novemba 27./Picha:Wengine

Iwapo atachaguliwa, Profesa Janabi atachukua nafasi ya Faustine Ndugulile aliyefariki dunia nchini India wakati akipatiwa matibabu.

Kwa sasa, Profesa Janabi ambaye amejizolea umaarufu nchini Tanzania kutoka na mafunzo yake ya lishe bora, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, akiwa pia ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais wa masuala ya afya.

TRT Afrika