Maafisa wa serikali ya Nigeria wameikashifu Canada kwa kuwanyima viza baadhi ya maafisa wakuu wa kijeshi akiwemo afisa wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi nchini humo.
Christopher Musa, Mkuu wa Majeshi, alisema ujumbe huo ulikuwa umeratibiwa kuhudhuria hafla ya kuwaenzi maveterani wa jeshi waliojeruhiwa wa Nigeria.
"Nusu ya timu yangu... tayari wamekwenda," Musa alisema katika tukio katika mji mkuu wa Abuja Alhamisi.
Lakini ubalozi wa Kanada, "kwa ujuzi unaojulikana zaidi kwao, ulitunyima visa", aliongeza.
'Sababu za siri'
Ubalozi wa Kanada nchini Nigeria ulisema kwenye akaunti yake ya X kwamba unafahamu suala hilo lakini ukakataa kutoa maoni zaidi, ukitaja "sababu za faragha".
Musa hakutaja ni lini visa hivyo vilikataliwa, lakini Kanada ilitangaza Jumatano kwamba imeanzisha kanuni za ziada zinazowapa mamlaka maafisa wake "kughairi hati za wakaazi wa muda".
Hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa mpaka wa nchi na kuhakikisha uadilifu wa programu zake za visa.