Ni wakati wa kutafuta amani nchini DRC, asema Guterres wa UN

Ni wakati wa kutafuta amani nchini DRC, asema Guterres wa UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema DRC ina uhitaji mkubwa wa amani kwa sasa.
Kulingana na Guterres, mapigano kati ya vikundi vyenye silaha na kile cha M23, yamesababisha idadi kubwa ya vifo na watu wengi kukosa makazi./Picha: Reuters

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema kuwa kuna hitaji kubwa la upatikanaji amani nchini DRC.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Guterres alisema kuwa hali ya DRC kwa sasa inaogopesha, akiongeza kuwa ni wakati muafaka kwa ulimwengu “kuwa kitu kimoja na kusaka amani kwa ajili ya nchi hiyo."

"Suala la DRC litakuwa ni ajenda muhimu wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika kitakachofanyika mjini Addis Ababa wiki ijayo," alisema Guterres.

'Idadi kubwa ya vifo'

Kulingana na Guterres, mapigano kati vikundi vyenye silaha na kile cha M23, yamesababisha idadi kubwa ya vifo na watu wengi kukosa makazi.

"Hali kwa watu wa Goma siyo ya kuridhisha, huduma za afya zimeelemewa, " alisema.

"Ujumbe wangu ni huu: Tuache vita. Tuheshimu utawala wa DRC na tuimarishe sheria za kimataifa za haki za binadamu. Hakuna suluhisho la kijeshi," aliongeza.

TRT Afrika