Serikali ya Afrika Kusini ilithibitisha kukamatwa kwa mtoro wa jela, Thabo Bester na mwenzake Dkt Nandipha Magudumana wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumamosi.
“Waziri wa Polisi na Waziri wa Sheria wanaweza kuthibitisha kuwa mtoro huyo Bw. Thabo Bester... pamoja na msaidizi wake anayejulikana pia kwa jina la Dkt Nandipha Magudumana pamoja na raia wa Msumbiji wamekamatwa nchini Tanzania usiku wa kuamkia jana. ," Waziri wa Sheria Ronald Lamola alisema.
Waziri wa Sheria Ronald Lamola alisema alikuwa na mazungumzo ya simu na mwenzake wa haki nchini Tanzania ambapo wawakilishi "walithibitisha kwetu ushirikiano wao na nia ya kusaidia kuwaleta Afrika Kusini haraka iwezekanavyo".
Msemaji wa Polisi nchini Tanzania kupitia taarifa kwa vyombo vya habari alithibitisha kuwa makachero wamewakamata Thabo Bester na Zakariah Alberto pamoja na Dkt Nandipa Madugumana.
Bester ni mkimbizi anayesakwa kufuatia kutoroka kwa kina kutoka kwa Gereza la Mangaung huko Bloemfontein mnamo Mei 2022.
Hivi majuzi polisi walivamia jumba la kifahari katika kitongoji cha Hyde Park huko Johannesburg, ambapo Bester na Magudumana walikuwa wamejificha.
Bester alikuwa akitumikia kifungo kwa ubakaji na mauaji.