Mkenya Peres Jepchirchir alivuk autepe mbele ya Buckingham Palace   kwa saa mbili dakika 16 sekunde 16 na kuvunja rekodi ya Mary Keitany ya 2:17:01 kwa wanawake.

Bingwa mtetezi wa Olimpiki Peres Jepchirchir alivunja rekodi ya dunia ya wanawake pekee katika kushinda mbio za 44 za London Marathon siku ya Jumapili, huku Mkenya Mkenya Alexander Mutiso Munyao akikimbia na kushinda katika mbio za wanaume.

Jepchirchir mwenye umri wa miaka 30 alitifua kivumbi katika mita 300 za mwisho, na kuvuka mstari wa mwisho mbele ya kasri la Buckingham kwa saa mbili dakika 16 sekunde 16 na kuvunja rekodi ya Mary Keitany ya 2:17:01 kwa wanawake. -shindano pekee katika hafla ya London ya 2017.

Mkenya Alex Munyao alimiuonyesha kivumbo mkimbiaji nguli wa Ethiopia Kenenisa Bekele na kuvuka utepe kwa  2:04.01. /Picha : World Athletics 

Munyao, 27, alionekana kusherehekea kwa kurusha ngumi angani mara kadhaa akielekea kwenye ushindi mkubwa zaidi wa maisha yake, akijiondoa kutoka umbali akimuacha nyuma mkimbiaji nguli Kenenisa Bekele na kuvuka saa 2:04.01.

Bekele wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 41 - ambaye amekimbia kunyakua mataji matatu ya Olimpiki kwenye barabara wazi na mataji 17 ya dunia katika mbio za nje na za ndani na za Cross country - alishika nafasi ya pili kwa muda wa 2:04.15, huku Muingereza Emile Cairess akishika nafasi ya tatu. 2:06.46.

Salamu za pongezi kwa Wakenya hao zilisambaa katika mtandao wa X, huku shirika la riadha Kenya , Athletics Kenya, likituma imoji za moto, kuonyesha kuwaka kwa nyota hao nakuongeza ujumbe hongera.

Waziri wa michezo wa Kenya Ababu Namwamba pia aliwatumia ujumbe wa pongezi nyota hao wa Kenya.

''Mbio ya kiwazimu kabisa hadi kukata utepe , Peres! Inasisimua kabisa,'' aliandika Waziri Namwamba. ''Maandalizi mazuri ya Michezo ya Olimpiki ya Paris ya Majira ya joto, ambapo pia utakuwa ukitetea taji lako kutoka kwa Olimpiki ya Tokyo,'' aliongeza Namwamba.

''Hongera Munyao, mumeinua jina la Kenya katika barabara za London baada ya Mkenya mwenzako Jepchirchir kuvunja rekodi ya wanawake huko,'' ilisema ujumbe wa waziri Namwamba katika ukurasa wa X.

Tigst Assefa wa Ethiopia, aliyetumia saa 2:11.53 katika mbio za Berlin Marathon mwezi Septemba na kuweka rekodi ya dunia kwa wanawake katika mbio pamoja na wakimbiaji wanaume, alivuka nafasi ya pili katika mbio za wanawake kwa saa 2:16.23.

Joyciline Jepkosgei wa Kenya, mshindi wa London 2021, alikuwa wa tatu kwa 2:16.24.

Taasisi ya rekosi za dunia Guiness World Record, ilimkabidhi bingwa huyo wa Kenya Peres Jepchirchir taji lake papo kwa hapo huku ikimpongeza kwa ushupavu wa hali ya juu.

Peres Jepchirchir akipokea taji la ubingwa wa dunia la Guiness World record / Picha: Guiness World Record 
TRT Afrika na mashirika ya habari