Misri yasema foleni katika mfereji wa Suez ni kawaida baada ya meli ya mafuta kuharibika

Misri yasema foleni katika mfereji wa Suez ni kawaida baada ya meli ya mafuta kuharibika

Meli ya mafuta yenye alama ya Malta yaharibika, na kusababisha kwa muda msongamano katika Mfereji wa Suez
Mamlaka ya Mfereji wa Suez (SCA) ilisema meli ya mafuta yenye bendera ya Malta ya SEAVIGOUR iliharibika baada ya kupata hitilafu / Photo: Reuters

Misri ilisema Jumapili kwamba shughuli katika mfereji wa Suez zimerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuiondoa meli ya mafuta ambayo iliharibika na kutatiza kwa muda msongamano katika njia hiyo muhimu ya maji duniani.

Katika taarifa, Mamlaka ya Mfereji wa Suez (SCA) ilisema meli ya mafuta yenye bendera ya Malta ya SEAVIGOUR iliharibika baada ya kupata hitilafu ya injini kwenye eneo la umbali wa kilomita 12 wa mfereji huo.

Mwenyekiti wa SCA Admiral Osama Rabie alisema meli hiyo ilikuwa sehemu ya msafara wa kaskazini, ambao unapitia mfereji kutoka Mediterania hadi Bahari Nyekundu.

Alisema boti za kuvuta zilitumwa kuvuta meli hiyo yenye urefu wa mita 274 na upana wa mita 48, na kuruhusu usafiri katika njia hiyo muhimu ya maji kurejea katika hali ya kawaida.

Rabie alisema meli hiyo ya mafuta, iliyokuwa ikitoka Urusi kuelekea China ikiwa na uzito wa tani 82,000, itaanza safari yake baada ya wafanyakazi wake kurekebisha hitilafu.

Mfereji wa Suez ni njia ya kimkakati ya maji inayounganisha Bahari ya Mediterania na Bahari ya Shamu, na inachukuliwa kuwa chanzo kikuu cha fedha za kigeni kwa Misri.

Mwezi uliopita, mamlaka ya Misri iliikwamua shehena nyingine ya mizigo iliyokuwa imekwama kwa saa kadhaa kwenye njia ya maji.

AA